Warembo 18 watakaoshirki kinyanganyiro cha kumtafuta Redds Miss Ilala wataondoka Jumamosi asubuhi kuelekea Tanga kwa ziara ya siku mbili ya kimafunzo ambapo watahudhuria pia shindano la kumtafuta mlimbwende wa mkoa wa Tanga. Wakiwa katika jiji la Tanga watatembelea vivutio vya utalii vya mji huo ikiwa ni kwenda katika mapango ya Amboni, kutembelea fukwe na sehemu nyingine za jiji hilo.Warembo hao wataongozana na Mwalimu wao Leila Bhanji, Matron Leila Bhanji na Viongozi wa kamati ya Miss Ilala.
Warembo wa Ilala pia watahudhuria sherehe za ufunguzi wa mashindano ya magari yatakayofanyika Jumapili katika jiji hilo.
Huu ni mwaka wa tatu mfululizo, warembo wa Ilala wakifanya safari kama hizi za Kitalii na mafunzo. Mwaka jana, Kampuni ya Dar Metropolitan Promotions inayoandaa mashindano ya kumtafuta mrembo wa Ilala iliwapeleka warembo katika mbuga za wanyama za Manyara na Tarangile zilizoko Mkoani Arusha.
Warembo wetu wameiva tayari kwa shindano shindano litakalo fanyika wiki ijayo tarehe 26/6/2010 katika ukumbi wa Ubungo Plaza. Sasa kinachofanyika kwenye kambi ni kuimarisha na kuendeleza vipaji vyao tayari pia kwa shindano la kupima vipaji litakalo fanyika mapema wiki ijao ambapo litahudhuriwa na waalikwa tu,
Kwa kweli ni vyema tuwashukuru wadhamini wetu ambao wamefanikisha mpaka sasa hivi maandalizi yetu ingawa bado kuna mapungufu kadhaa.ambayo yanatufanya kutokufunga milango kwa wadhamini wengine. tunawakaribisha.
Wadhamini wetu mpaka sasa ni Redds Original Premium ambao ni wadhamini wakuu, wengine ni Vodacom Tanzania, Aurora Security, Muzasha tours and Safaris, PSYSCORP group, Channel Ten and Magic FM, Valye Spring, Habari Leo, Fullshangwe blog, Sofia Records na Clouds FM

No comments:
Post a Comment