HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 30, 2010

Siku Ya Familia Kwa Wafanyakazi Wa TBL

Mkurugenzi wa Ufundi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Trevor Gray (kulia) akimzawadia mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo box moja la kilaji cha safari lager Siku ya Familia za wafanyakazi wa kampuni hiyo, iliyofanyika katika Hoteli ya South Beach, Kigamboni, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
wakiwa wametulia kivulini huku wakidiskasi mambo mawili matatu
Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na familia zao, wakishindana kuvuta kamba wakati wa Siku ya Familia iliyofanyika katika Hoteli ya South Beach, Kigamboni, Dar, wikiendi ilopitaMkurugenzi wa Ufundi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Trevor Gray akimpongeza mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo, aliyeshinda mbio za Km 2 katika tamasha la Siku ya Familia ya wafanyakazi wa kampuni hiyo, iliyofanyika katika Hoteli ya South Beach, Kigamboni, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kutoka kulia ni Ofisa Uhusiano Lillian Erasmus, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Uhusiano, Steven Kilindo, Meneja wa Kiwanda, Salva Rweyemamu na Meneja Miradi Clinton Kimber.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania na familia zao wakipata mlo wa mchana wakati wa Tamasha la Siku ya Familia iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya South Beach Mfanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Sufiani Athuman, akishindana kucheza pool na mfanyakazi mwenzie Rajabu (hayupo pichani) katika pambano lililofanyika Siku ya Familia iliyofanyika katika Hoteli ya South Beach, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Wa pili kushoto ni mwamuzi wa pambano hilo, Skubi Mlapakolo.
michezo mingi ilichezwa siku hiyo ukiwepo huu.
Familia za wafanyakazi wa kampuni ya bia TBL zikijinafasi.

1 comment:

Post Bottom Ad