
Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia wanachama wa CCM katika mkutano huo leo

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya wanachama wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam waliojitokeza kumdhamini katika fomu za kuomba kuteuliwa kugombea Urais, leo kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam.

Ridhiwani Kikwete (wa pili kushoto) ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana waliopewa jukumu la kuratibu shughuli ya kutafuta katika mikoa kumi wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wa kumdhamini Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete katika fomu za kuomba kuteuliwa kugombea Urais, akijadiliana jambo na baadhi ya vijana wa chama hicho.

Baadhi ya wanachama wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, wakimshangilia Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani) wakati akiingia kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza jana,kuzungumza na wanachama 350 waliojitokeza kumdhamini kwa kujaza fomu za kuomba kuteuliwa kugombea Urais, leo kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam.
Hawa watu wananichosha ni kweli wanafuraha au kujipendekeza tu.
ReplyDelete