HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 10, 2010

miss dar indian ocean kufanyika june 10

washiriki wa Miss Dar Indian Ocean wakiwa katika picha ya pamoja

Miss Dar Indian Ocean iliyoko chini ya maandalizi ya Frontline Management imepangwa kufanyika wiki hii tarehe 10th Mwezi wa 6 katika hotel at Double Tree Hilton.


Mpaka sasa kambi ya Miss Dar India Ocean ina wasichana 12 ambao ni Irene Haule (20), Jacqueline Madundo (20), Esthet Flavian (20), Rose Masanja (22), Nurie Ahmed (18), Ramla Mohamed (19), Happy Whitney Andrew (19), Edna Kwilasa (22), Irene Hezron (22), Winnie Richard (20), Aneth Brayson (23), Rehema Faraji (22), Magreth Hussein (18) and Alice Lushiku (23).

Kambi hii ilianza tarehe 2 June na imehusishaa shughuli mbali mbali kama mafunzo ya uvaaji, kujiremba, HIV/AIDS, ushauri nasaha, uongozi, unadhifu na maswala ya jamii.

Vile vile warembo wa kitongoji hiki wanatarajia kutembelea kituo cha watoto yatima cha Mitindo House ambako watapaka kituo hicho rangi kwa hisani ya Robiallac.

Mshindi wa Dar Indian Ocean atapata Tshs. Million 1.2, ikifuatiwa na Tshs. Laki 8 kwa mshindi wa pili, laki 5 kwa mshindi wa tatu na laki moja moja kwa washindani waliobaki.

Shindano hili limedhaminiwa na Vodacom, Redds, Robiallac na Shear Illusion, na tiketi zanapatikana kwenye maduka yote ya Shear Illusion na kwenye ofisi za Frontline Management zilizopo Kinondoni kwa Tshs. 30,000 tu.

Nancy Sumari, meneja wa matukio kwenye kampuni ya Frontline Management amesema “nia kubwa sana ya kujihusisha kwenye uandaaji wa mashindano haya ya Miss Tanzania ni kuhakikisha kwamba washiriki wanapewa mwongozo na support itakayowawezesha kumudu presha zinazowakumba wanaposhinda taji.

Hii itasaidia kupunguza skendo zinazowakumbaa mamiss na kuwawezesha kuwa na mwelekeo wa kimaisha” Sumari aliendelea kusema kuwa shoo ya kumpata mrembo wa Dar Indian Ocean itakuwa ya kuvutia na kuburudisha sana.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad