Zawadi Msalla na Jovina Bujulu
-
MAELEZO DODOMA.
JESHI la Polisi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania lipo katika mchakato wa kubadilisha mfumo wa utoaji leseni za udereva kwa kuanza kutoa leseni za elektroniki.
Hayo yameelezwa leo Bungeni na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Lawrence Masha, alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2010/2011.
Waziri Masha alisema lengo la mpango huo ni kuhakikisha kumbukumbu za madereva kote nchini zinawekwa kwa usahihi hivyo kupunguza ukiukwaji wa sheria barabarani na utoaji holela wa leseni bandia nchini.
Masha alisema mpango huo utatekelezwa katika awamu mbalimbali ambapo awamu ya kwanza inatarajiwa kuanza mwezi Septemba mwaka2010 katika vituo tisa vya Arusha,Kilimanjaro,Tanga,Mbeya,Dodoma, Mwanza,Ilala Temeke na Kinondoni.
Masha alisema katika mabadiliko hayo leseni zitaongezeka kutoka aina nane zilizopo sasa na kufikia kumi na nne na zitakuwa na fursa ya kuweka kumbukumbu zote muhimu zinazotakiwa na kuongeza kuwa leseni hizo hazitakuwa rahisi kughushika.
Aidha Waziri alisema zoezi hilo litaenda sanjari na uhakiki wa leseni za udereva za daraja C ambapo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Wizara ya Miundombinu na Mamlaka ya Mapato litaanza zoezi la kuhakiki umiliki wa leseni za udereva daraja la C kwa lengo la kubaki na wamiliki wale tu wenye sababu za msingi za umiliki wa leseni hizo.
Alisema kwamba wapo wananchi wengi wanaomiliki leseni hizo kinyume na taratibu na sheria za barabarani kwani leseni hiyo ya udereva inaruhusu uendeshaji wa magari aina zote na pikipiki yakiwemo mabasi ya abiria.
Masha aliongeza watakao onekana hawana sababu za msingi za kumiliki aina hiyo ya leseni watapatiwa leseni ya udereva daraja B au D.
Waziri aliwaasa madereva kote nchini kuzingatia sheria za barabarani ili kupunguza idadi ya ajali za barabarani zinazoendelea kuzidi siku hadi siku.

No comments:
Post a Comment