HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 27, 2010

Singida Yaingia Fainali Kwa Kuitandika Arusha Bao 3 - 2

mshambuliaji wa timu ya Singida,Kelvin Charles (10) akijaribu kumtoka beki wa timu ya Arusha,Saidi Mussa (4) katika mchezo wa hatua ya nusu fainali ya kwanza iliyochezwa leo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar.Singida imeshida 3 - 2 dhidi ya Arusha.kwa matokeo haya ni kwamba timu ya Singida imetinga fainali na inasubiria timu moja wapo kati ya Lindi na Ilala zitakazopigwa kesho katika uwanja wa Uhuru jijini Dar.
wachezaji wa timu ya Singida wakimpongeza mwenzao baada ya kufunga goli ya pili.
mshambuliaji wa timu ya Arusha,Abdallah Salum (9) akikontroo mpira mbele ya beki wa Singida,Burhani Hamis (3) katika mchezo wa nusu fainali wa mashindano ya Kiti Taia Cup uliochezwa jioni ya leo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar.Singida imechapa Arusha bao 3 - 2
mmmhhh.... hii sio faulo kweli??
mchezaji wa Singida,Kelvin Charles (10) akiwazungusha mabeki wa timu ya Arusha.


madogo wakijisevia vigudulia vya maji ya kunywa vilivokwisha tumika kwaajili ya kwenda kuvipiga bei.hali hii ya madogo hawa ndio inanikumbusha ule usemi usemao "rizki fil manyati" yaani rizki ni lazima uinyatie ndio uipate.kweli waliosema hili hawakukosea hata kidogo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad