HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 31, 2010

Sherehe Za Kutolewa Kwa Tuzo Kwa Bidhaa Bora Duniani Zaanza Huko Nchini Ujerumani

Kushoto ni Bw. Edwin Gafa, kiongozi wa msafara wa Nile Breweries ya Uganda ambao wamepata tuzo ya kushiriki mara nyingi kwenye Monde Selection, Wawakilishi wa kampuni ya TBL ,Meneja wa Ndovu Lager Oscar Shelukindo akiongozana na Mpishi mkuu wa kampuni hiyo (Chief Brewer) Gaudence Mkolwe.
Meneja wa Ndovu Lager Oscar Shelukindo (TBL) pamoja na Mpishi mkuu wa kampuni hiyo (Chief Brewer) Gaudence Mkolwe wakiwa na bidhaa yao ya Ndovu ambayo leo jumatatu usiku itapokea tuzo ya Dhahabu kwenye sherehe za ubora wa bidhaa za Monde Selection ambazo zimeanza rasmi katika ukumbi wa Kurhaus jijini la Wiesbaden, Ujerumani usiku wa kuamkia leo, ambapo makampuni kibao toka kile pembe ya Dunia ambayo bidhaa zake zimeibuka kuwa washindi wa ubora yatazawadiwa.
Mpishi mkuu wa kampuni ya TBL (Chief Brewer) Gaudence Mkolwe akiangalia vinywaji mbalimbali vilivyopo kwenye sherehe za ubora wa bidhaa za Monde Selection ambazo zimeanza rasmi katika ukumbi wa Kurhaus jijini la Wiesbaden, Ujerumani usiku wa kuamkia leo, ambapo makampuni kibao toka kile pembe ya Dunia ambayo bidhaa zake zimeibuka kuwa washindi wa ubora yalizawadiwa.
Meneja wa Ndovu Lager Oscar Shelukindo (TBL) akiangalia moja ya kinywaji kilichoibuka kwenye ushiriki wa kunyakua tuzo usiku wa kuamkia leo,ambapo hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Kurhaus mjini Wiesbaden,chini Ujerumani. Meneja wa kinywaji cha Ndovu Oscar Shelukindo na mpishi mkuu wa TBL Gaudence Joseph Mkolwe wakiwa nje ya ukumbi wa Kurhaus jijini la Wiesbaden, Ujerumani usiku wa kuamkia leo
Sherehe za ubora wa bidhaa za Monde Selection ambazo zimeanza rasmi katika ukumbi wa Kurhaus jijini la Wiesbaden, Ujerumani usiku wa kuamkia leo, ambapo makampuni kibao toka kile pembe ya Dunia ambayo bidhaa zake zimeibuka kuwa washindi wa ubora yatazawadiwa
Wageni waalikwa kutoka makampuni mbalimbali wakiwa ndani ya ukumbi wa Kurhaus jijini la Wiesbaden, Ujerumani usiku wa kuamkia leo.
Oscar na Mzee Mkolwe wakiwa katika jumba la Kurhaus mjini Wiesbaden wikiendi hii ambako sherehe za Monde Selection za kutuza bidhaa bora duniani zinafanyika. Tuzo ya Dhahabu iliyopata kilaji cha Ndovu inatolewa jioni ya leo katika ukumbi huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad