HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 25, 2010

Lindi Na Ilala Zatinga nusu fainali Kili Taifa Cup

mshambuliaji wa kushoto wa timu ya Iringa,Brington Mponzi (15) akijaribu kuwatoka mabeki wa timu ya Ilala,George Minja (kushoto/15) na Shaban Sunza katika mchezo uliochezwa mchana wa leo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar.Ilala imeshindwa kwa mikwaju ya penati 5 -3 dhidi ya Iringa
mshambuliaji wa timu ya Lindi,Ally Mohamed "Gaucho" (10) akijaribu kutaka kumtoka beki wa timu ya Kilimanjaro,Emmanuel Lugano huku akisaidiwa na Raphael Mhanga katika mtanange uliopigwa jioni hii katika uwanja wa Uhuru.Lindi imefanikiwa kusonga mbele kwa hatua ya nusu fainali mara baada ya kutandika timu ya Kilimanjaro mabao 3-1.magoli ya Lindi yalifungwa na Ally Mohamed "Gaucho" (26),Aman George (34 kwa mkwaju wa penati) na Omar Matwiko alimalizia kwa goli la tatu.huku kwa upande wa Kilimanjaro goli lilifungwa na Magogo Mgaya.
Nyanda wa Ilala akishangilia baada ya kuiwezesha timu yake kusonga mbele kwa hatua ya nusu fainali baada ya kucheza penati mbili leo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar.
kocha wa timu ya Ilala Jamhuri Kihwelo "Julio" akihojia na mtangazaji mahiri wa ITV,Isack Gamba mara baada kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Iringa leo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar.
Nyanda wa Kilimanjaro Emmannuel Mseja akishuhudia kitu kikitinga wavuni.
Athuman Iddy Chuji wa Iringa akiwania mpira wa juu na beki wa Ilala,Shaban Sunza katika mchezo uliopigwa mchana wa leo katika uwanja wa Uhuru.Ilala Imeweza kusonga mbele kwa hatua ya nusu fainali baada ya kufunga Iringa kwa mikwaju ya penati 5 - 3.
mpira ukikokotwa kuelekea langoni kwa Ilala.
mambo ya faulo hayooo.pale ni Chuji na Swedi wa Iringa wakiwachanganya wapinzani wao ambao ni Ilala waliojipanga kukinga mpira huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad