HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, April 25, 2010

Wimbo Wa Taifa Rimix.........!!!!??

Wadau naomba mnisaidie jambo moja juu ya Wimbo wa Taifa.
Leo nilikuwa viwanja vya Mnazi Mmoja katika Siku ya Maleria, Mgeni rasmi alikuwa Rais Jakaya Kikwete.

Rais alipowasili tukasimama kuimba wimbo wa taifa na wimbo huo uliimbwa na msichana mmoja nafikiri ni kutoka THT lakini kiukweli ule haukuwa Wimbo wa Taifa la Tanzania ambalo mimi na wewe tupo na tunajivunmia kuwa watanzania.

Wimbo ule naweza kusema ni Rimix ya Wimbi halisi wa taifa ambao wengi tunaujua maana si sauti wala ala ya muziki ambayo inafanana na Wimbo halisi wataifa.

Swali ni je inakuwaje tunaandaa shughuli ya Kimataifa/ kitaifa kama ile ya leo na Mgeni rasmi ni Rais wa nchi halafu tunaimba Wimbo ambao sio wataifa?, Wahusika kuanzia ngazi ya maofisa utamaduni na idara zote wanakuwa wapi hadi wimbo kama huu kuruhusiwa kuimbwa kwa heshima na Rais akiwa amesimama ambao hauna sifa ya kuwa Wimbo wa taifa?.

Sikuwahi fikiria kama nchi hii tunaweza kubadili vitu kiasi hiki na kuvifanya mbele ya Rais. Tena nasikia kuna siku ya Uzinduzi wa MALERIA HAIKUBALIKI pia uliimbwa wimbo huo tena vibaya zaidi afadhali ya leo kwa aliyesikia awali japo mimi nasema sio wimbo wa Taifa. Kwanza ni lini mtu mmoja akatuimbia wimbo wa taifa? na hata mtoto wa darasa la kwanza akiiimba wimbo wa taifa hata uimba vibaya kama ulivyoibwa.

Ama ni kutokuelewa kwangu huenda ndo Wimbo maalum wa Tiafa katika Kupiga vita Maleria.

Alamsiki.
Father Kidevu
www.mrokim.blogspot.com

1 comment:

  1. father kidevu ungetuweke link hapa na sisi wa mbali tuweze kuusikia na ku comment.
    we also need to hear the so called wimbo wa taifa remix ....

    kama ni kweli basi tumeishiwa .

    kwishnei .

    uzalendo umeisha jamani .
    mdau no 5 .

    ReplyDelete

Post Bottom Ad