***
Jana usiku nimeanza kusoma kitabu cha mwandishi maarufu, John Grisham. Kitabu kinakwenda kwa jina la "The King of Torts". Nimesoma sura mbili tayari na kwa kweli kimenibamba, nikasema itakuwa si vibaya nikishirikiana uhondo huu na wanakijiji wenzangu, ila ukitaka uhondo halisi ukipate kitabu chenyewe.
Katika King of Torts anazungumziwa mwanasheria mmoja wa serikali, Clay Carter, ambaye amekabidhiwa jukumu la kusimamia kesi ya dogo mmoja anayekwenda kwa jina la Tequila.
Usiku mmoja Tequila, kijana wa miaka 20, anampiga risasi ya kichwa kijana mwingine anayekwenda kwa jina la Pumpkin. Mauaji haya yanashuhudiwa na watu wasiopungua wanane. Mauaji haya yanatokea katika kona ya mtaa wa Georgia na Lamont, huko Washington D.C, Marekani.
Milio ya risasi katika mtaa huu uliojaa watu wenye umasikini mkubwa ni jambo la kawaida. Lakini pamoja na mauaji kutawala mitaa hii, risasi inayofyatuliwa na Tequila usiku huu bado inawafanya watu kukimbilia majumbani mwao na kujifungia.
Kati ya watu nane wanaoshuhudia Tequila akishindilia risasi katika utosi wa Pumpkin ni masela fulani wawili ambao walikuwa wameketi nje ya duka moja la bidhaa za nyumbani. Baada ya uhai kumtoka Pumpkin, Tequila anawafata hawa jamaa, nia yake ni kutaka kuwamaliza ili kupoteza ushahidi. Jamaa wanafanikiwa kutoka baruti (kukimbia). Tequila anaondoka zake eneo la tukio akiwa na bastola yake mkononi, cha kushangaza ni kwamba jamaa anaondoka kwa mwendo wa kawaida tu, kama vile hakuna kilichotokea.
Masela wale wawili waliotoka baruti wanafanikiwa kupiga simu polisi na kuwaarifu kuhusu mauaji yaliyotekea hivi punde. Masaa matatu baadae polisi wanafanikiwa kumtia mbaroni Tequila akiwa kama mtaa wa tatu hivi toka pale alipofanyia mauaji. hata hivyo kwa wakati huu Tequila hana silaha aliyofanyia mauaji.
Polisi wanarudi na Tequila hadi kwenye maiti ya Pumpkin. Kwa muda wote huu tangu polisi wamtie dogo mbaroni, dogo hajafungua mdomo wake kusema neno hata moja, hata baada ya polisi kutishia kumtesa. Wanapofika katika maiti ya Pumpkin wale masela waliopiga simu polisi, pamoja na wale watu wengine sita walioona mauaji yale yakitendeka wanawathibitishia Polisi kwamba Tequila ndio hasa muuaji, kwani nguo alizokuwa amevaa wakati anampeleka Pumpkin kuzimu, ndio zilezile alizovaa hadi sasa. Tequila anatupwa lupango kusubiri kupelekwa mahakamani siku inayofuta.

Baada ya polisi kumsweka Tequila rumande, inawachukua masaa yasiyopungua sita kugundua kwamba marehemu Pumpkin hana baba, na hata kama yupo hakuwahi kumtia machoni. Wanapopeleleza zaidi wanagundua kwamba Pumpkin amabaye ndio kwanza alikuwa yuko kwenye miaka yake ya mwanzo ya 20, alikuwa akiishi na mama yake pekee, wanagundua pia kwamba jina halisi la jamaa ni Ramon Pumphrey, Pumpkin lilikuwa jina lake la utani tu. Mama yake ni mlinzi katika kampuni moja kubwa hapo D.C.
Polisi wanafanikiwa kumpata mama huyu, jina lake kamili ni Adelfa Pumphrey. Mama ni kipande cha mtu, wanamkuta akiwa ameketi katika meza yake ya kazi, kiunoni ana mguu wa kuku (bastola). Polisi hawa wanaonekana kama wameshazoea kazi ya kuwafahamisha watu kwamba ndugu zao wamekutwa wamekufa, kwani wanapokutana na Adelfa haiwachukui hata sekunde kadhaa wanapasua jipu.
Looo, Adelfa pamoja na ujasiri wote alio nao na bunduki kiunoni, anaketi kitini na kukata chozi kuliko maelezo. Ukweli ni kwamba Adelfa ameshaona wazazi wengine wakipoteza watoto wao kwa mauaji ya kinyama hapa D.C, wazazi wengine ni rafiki zake wa karibu. Kila siku amekuwa akiwaza kwamba mauaji kama hayo yanaweza kugonga hodi nyumbani mwake, lakini leo habari hizi zinapomfikia ni kama hakuwa amejitayarisha. Mtoto kwa mama ni mtoto tu.
Polisi wale wanaondoka zao kama vile hakuna kilichotokea, wanamwacha Adelfa akilia kwa uchungu, akiapa kulipa kisasi kwa huyo aliyechukua maisha ya mtoto wake kipenzi, Pumpkin. Analaumu kifo hiki kwamba kimesababishwa na baba mtu kuikimbia familia yake na Pumpkin kukosa mapenzi ya baba. Juu ya yote anajipa moyo kwamba hali hii itapita.

Siku inayofuata Adelfa anajivuta Mahakamani, ameongozana na kaka pamoja na jirani yake. Baada ya muda mfupi mahabusu wanaanza kuingizwa mahakamani ili kusomewa mashitaka yao. Kati ya mahabusu hawa yupo Tequila ambaye tofauti na mahabusu wengine yeye amefungwa pigu mikononi na miguuni, kwani kosa lake ni kubwa zaidi. Mpaka muda huu polisi hawajafanikiwa kumfanya Tequila kufungua mdomo wake na kusema kwa nini ametoa uhai wa Pumpkin.
Adelfa anapomwona Tequila hasira zinampanda, anataka kusogea karibu na kumwuliza kwa nini ametwaa maisha ya mtoto wake lakini anajua wazi kwamba hawezi kupata wasaa huo.
Askari jela aliyemleta Tequila mahakamani anamweleza dogo kwamba mama wa marehemu ameketi kiti cha nyuma kabisa cha mahakama. Tequila ambaye alikuwa ameinamisha uso wake chini muda wote anatazama upande alioketi Adelfa, haoneshi kujutia alichofanya, anarejesha uso wake na kuendelea kutazama chini.
Jaji anaingia na kuanza kupitia mafaili ya watuhumiwa. Anapofikia faili la Tequila anaita, "Tequila Watson", dogo anasimama na kuitikia jina lake. "Unatuhumiwa kwa mauaji", Jaji anasema na mahakama nzima inakuwa kama imepigwa ganzi, kila mtu anaanza kusikiliza kwa makini. "Una umri gani?" Jaji anauliza, "Miaka 20" Tequila anajibu.
"Una uwezo wa kujiwekea mwanasheria?"
"Hapana"
"Nilihisi hivyo tangu awali" Jaji anasema kwa sauti ya chini, "Mahakama itakuwekea mwanasheria wa serikali". Anatazama huku na huko, hakuna mwanasheria hata mmoja, ghafla anamwona Clay Carter, ambaye ni mwanasheria wa serikali. Carter nae amegundua kwamba yuko peke yake humu mahakamani, wakati kwa kawadia huwa panakuwa na wanasheria wasiopungua 20 kwa wakati mmoja.
Carter ametoka kumaliza kesi ya mauaji iliyokuwa ikimkabili mtu mwingine siku za hivi karibuni, kesi hii imemgharimu muda wa miaka mitatu. Siku mtuhumiwa alipokutwa na hatia na kupeleka jela, Carter aliona kama ametua mzigo mkubwa, japo alikuwa akimtetea mteja wake.
"Mr. Carter" Jaji akamwita, haikuwa sauti ya kuamrisha bali ya kumsihi asogee katika meza ya Jaji. "Tafadhali shughulika na kesi hii" Jaji akasema huku akimkabidhi Carter kijifaili chembamba chenye maelezo ya kesi ya Tequila. Baada ya kukipitia haraka Carter akamwambia Jaji, "Mteja wangu hana hatia." Maneno ya Carter hayakuendana kabisa na muonekano wa mteja wake, kwani hata angesema anayo hatia, Tequila asingejali, ni kama alikuwa tayari kwenda jela. "Asante sana Mr. Carter", Jaji akasema huku akifungua faili la mtuhumiwa mwingine.
Carter anasogea na kuketi karibu na mteja wake. Anaanza kuchukua maelezo ya Tequila ambayo yalikuwa ni mafupi mno, mteja mwenyewe anaona kama wanampotezea muda tu. Carter anamuahidi Tequila kwamba atafuta melezo zaidi siku inayofuta huko kwenye seli yake. Anaondoka zake kurejea kwenye kijiofisi chake wakati Tequila akirejeshwa mahabusi.
endelea endelea kusoma sehemu ya pili ya simulizi hii kwakubofya HAPA>>>>>...

No comments:
Post a Comment