
katika katiza katiza zangu za Mtaa Kwa Mtaa,leo nikajikuta nimeibukia pande hii ya kkoo mtaa wa aggrey,mtaa ambao kwa sasa ndio umeshika kasi kweli kweli kwa biashara ya zile simu za kinanihii na zile zingine za orijino na kuwakuta kina mama hawa wajasilia mali wakiwa wamepanga laini za simu (SIMCARD) katika vibox mithili ya vitumbua na maandazi ya wale kina mama wa pale mtaani kwetu.nikajiuliza hivi inakuwaje hapa?? maana sasa hivi makampuni yoote ya simu hapa nchini yako katika zoezi la kusajiri namba zote za wateja wao na wameweka muda kabisa wa kusitishwa kwa zoezi hilo la usajiri.lakini huku mtaani bado hizo laini zimemwagwa kama njugu.sasa sijui itakuwa vipi????
No comments:
Post a Comment