
mshindi wa leo ni Irene toka pande za kule nanihii akiwa ameshika zawadi yake

Dj Mully B ndie alitoa zawadi hiyo kwa leo na hapa akiikabidhi kwa muhusika huku mdhamini wa zawadi hiyo akiangalia.

Afisa Mauzo wa Overmeer Wine (jina limenitoka kidogo) akiwa na mshindi wa kata nyonga a.k.a kizungushe kama unacho,aitwae Irene katika shindano linaloendelea kufanyika kila jumamosi katika usiku wa maflava ya ukweli pale mzalendo pub.

mzushi akiwa kapigwa na bumbuwazi pindi nyonga zikishindana kunyongwa.

mambo yamekoleaa

usipimeeeee

kitu mduariko,full nyomiii

mayenu kama kawa


zikipigwa zile za kiutu uzima utajua tuu,maana wahusika huwa hawajifichi hata kidogo.



mambo ya kwa mzee Madiba hayooooooo,nayo hayambagui mtu lazima ujiweke kati hapo ili nawe uweze cheza kwa stepu,yaani mbili kulia,mbili kushoto,unazungukaaa.yaani ni raha tupu ukiwa ndani ya Mzalendo pub katika usiku wa Flava.kama ulikosa wiki hii basi jitahidi wiki ijayo isikupige chenga maana utakuwa unakosa raha za dunia hiii bila sababi yoyote.
du mshikaji wangu hongera kwa kazi unayoifanya lakini washikaji wahusika wanaitambua kazi yako au, du mshikaji mbona gamba kazeeka hivyo kulikoni, mwambie mdau anasema punguza kilaji
ReplyDelete