.jpg)
KIKOSI CHA ZIMA MOTO KUWACHUKULIA HATUA WATU WOTE WATAKAO KAIDI AMRI YA KUNUNUA VIFAA VYA KUDHIBITI MOTO.
(Na Veronica Kazimoto – MAELEZO)
(Na Veronica Kazimoto – MAELEZO)
Naibu Kamishina wa Usimamizi na Uangalizi wa vikosi vya Zima moto na uokoaji Bwana Rogatius Kipali amesema ifikapo tarehe 30, Aprili mwaka huu watu wote ambao hawatakuwa wamenunua na kufungiwa vifaa vya kudhibiti moto – fire extinguisher, watalipa faini ya shilingi laki moja na kuendelea kulingana na ukubwa wa maeneo yao pamoja na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumza ofisini kwake jijini Dar leo, Bwana Kipali amesema zoezi hili litafanyika nchi nzima na faini hizo zitahusisha majengo yote, ofisi za Serikali na zisizokuwa za Serikali pamoja na maeneo ya biashara.
“Ni wajibu wetu kusimamia uwekaji wa vifaa vya kudhibiti moto kwenye majengo ya watu, ofisi, magari na maeneo yote ya biashara na kama watu hawatatekeleza agizo hili basi watatakiwa kutoa faini ya pesa tathilimu na wengine chukuliwa hatua za kisheria.” Amesema Bwana Kipali.
Kuhusu suala la uelimishwaji juu ya matumizi ya vifaa vya kudhibiti moto Bwana Kipali amebainisha kuwa mawakala wote waliopewa kibali cha kuuza na kufunga vifaa hivyo wana watalaamu ambao huwaelimisha wananchi namna ya kuvitumia na kuvitunza pindi wanapovinunua kutoka kwenye ofisi zao.
“Mawakala wote tuliowapa kibali cha kuuza na kufunga vifaa vya kudhibiti moto wana wataalamu wa kuwaelimisha wananchi namna ya kutumia vidhibiti moto na ndio wanaohusika kufunga vifaa hivyo kwenye maeneo ya wananchi na kuvifanyia ukarabati pindi huduma hiyo inapohitajika.” Ameongeza Bwana Kipali.
Amewataja baabhi ya mawakala waliopewa kibali kuuza na kufunga vidhibiti moto kuwa ni Adjef Intergrated LTD walioko Sinza A, Modern fire & General services walioko mtaa wa Miteja Temeke, Wino works LTD walioko mtaa wa Mafia Kariakoo na Sagom General Enterprises walioko mtaa wa Muhonda namba 9 Jangwani.
Wengine ni Unifarm Industrial Services walioko Mwanza mjini, Zanzibar Fire Protection Engineering walioko Amani Magogoni Zanzibar, Tradegate Investments walioko barabara ya Bagamoyo na taarifa za mawakala wengine hupatikana katika ofisi za zima moto zilizoko mikoa yote Tanzania.
Hata hivyo Bwana Kipali amekili kuwa mwitikio wa wananchi kununua vifaa vya kudhibiti moto ni mdogo sana hivyo anawaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kununua vifaa hivyo kwa mawakala walioko maeneo mbalimbali nchini kabla ya tarehe iliyotajwa hapo juu.
Agizo hilo la kununua na kufunga vifaa hivyo vya kuzima moto limefuatia kukithiri kwa matukio mengi ya moto nchini zikiwemo shule. Hivyo Serikali kupitia Jeshi lake la Zima Moto imejipanga kukabiliana na kutokomeza matukio hayo.

Ndugu watanzania wenzangu kifungu kipi cha sheria kinachomwozesha kamishna wa zima moto atoe amri kama hii ?? wasitufanye watanzania wajinga kwa wao kutupangia wapi kwa kununua vifaa hivyo kwa kuwa wao wanapata % yao, Amefanya vitu vingapi tangu aingie madarakani vya kuharakisha kupigana na majanga ya moto ? Kuna mabomba mangapi ya Emergency Fire pipe hapa mjini ? ..nchi hii imechafuka kila kiongozi anataka kuendesha nchi kivyake ..Tanzania Haijafikia hatua kubwa kama hiyo kwa nini wasianzie kwenye Majumba,maofisini mlango kwa mlango wanangangania kwenye magari ambayo risk yake ni ndogo compared na maofisi /nyumba !!! Huu ni uwizi mtupu ..na nashangaa waeshimiwa wamekaa kimya sababu wao hayawahusu . kwa nini wasianze kwanza na nyumba/majengo na magari ya serikari kabla ya kuja kwa wananchi ?? wao wanatakiwa kuwa mfano . Mbona wenzetu wa TCRA walipotoa amri ya kurejista number waliweka bila ya kuwa na cost na makampuni ya simu ndiyo yanayobeba cost nzima ya kurejista number , na kwa nini wao kufanya inspection lazima ulipie ? na fedha hizo zinakwenda wapi ndugu zangu ? JAMANI WADANGANYIKA TUSIBURUZWE KAMA WAFUNGWA WATAFUTE NJIA NYINGINE YA KUONGEZA MAPATO SISI WANANCHI WA KAWAIDA TUNABEBESHWA MZIGO MZITO WAKATI WAO SERIKARINI WANAENDESHA MAGARI YA KIFAHARI YENYE THAMANI KUBWA BILA YA KUWA NA VIFAA VYA KUZIMIA MOTO JE HII NI HALALI?????
ReplyDelete