HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 29, 2010

Somo Kwa Wana Hip Hop Toka Kwa Mwanalibeneke King Kif


Ndani ya Mtaa kwa Mtaa leo King Kif kutoka www.kingkif.blogspot.com namiminika na madude ya muziki wa Hip-Hop ambao hapo zamani hapa Bongo tuliuita muziki wa kufokafoka , hiyo ilikuwa mwishoni mwa miaka ya themanini na tisini mwanzanzoni.Basi bwana, hapa kwanza kabisa kunahitajika kufahamu nini maana ya sayansi na nini maana ya Philosophy.
Science means a techinique to simplify work which includes branches such as mathematics and a Geography

SAYANSI NA HIP-HOP

Sayansi na Hip-Hop ; Hip-Hop ni lazima iandikwe kwa kutumia mizani , hii ina maana lazima uwe na idadi maalum ya mizania katika mistari ili mashairi yako yaweze kuimbika(kuchanika).

Pia beats (midundo) ya Hip-Hop lazima igonge katika mahesabu maalum ambayo kwa Hip-Hop ni 4 (four) , hivyo hata mistari inahimizwa kuangukia kwenye hesabu hiyo hiyo ya vigawe vya 4(nue) yaani 4,8,12 na kuendelea .

Hapo tunaona wazi hesabu inavyotawala katika uhunzi mzima wa mashairi na beats(midundo) ili kufanya ama kujenga kitu kinachoitwa HipHop.


PHILOSOPHY

Means love anda wisdom (hekima na upendo ) , ni neno (lenye asili ya Kigiriki). Philo means love and Sophia means Wisdom.

Philosophy na Hip-Hop ; ni wazi kabia na haipingiki kwamba muziki huo unaleta upendo ikiwa ni pamoja na kutumika njia ya kuleta ama kudai haki , kukemea unyonjaji katika jamii na kadhalika.

Aidha, mistari ama mashairi bora ni yale yaliyo na hekima yasikilizwapo katika masiko ya watu na si vinginevyo , mfano ni mistari inayopatikana kwenye traki kali iitwayo " I know i can" ya Nas . Traki hii ina maneno ya hekima na upendo ndani yake juu ya maisha kuanzia utoto hadi utu uzima.

MIFANO MINGINE DHAHIRI

Hii hapa mifano mingine kadhaa ya watu ama niandike maemsii walioweza kujiita Hip-Hop mathematic ambao ni kama vile RZA ambaye ni kiongozi wa kundi mahiri la Wu Tang Clan , yupo Cani-Bus , yupo Mos Def .Pia yupo jamaa mmoja aitwaye Keith Muray wa kundi la DEF Squad na wengine wengi .

King kif kutoka www.kingkif.blogspot.com namaliza hapa huku nikisisitiza Hip-Hop bila Science $ Philoph ni pumba tupu na hata mashabiki hasa hapa Tanzania waufuatilie kwa undani muziki huu na waache ushabiki mandazi.

2 comments:

  1. Mwana hili ni dude mwake kabisaaa!

    ReplyDelete
  2. Tukipata makala kali ya kiswahili nyingine kama hii kuhusu Hip-Hop mbona upewe utaongezeka!

    ReplyDelete

Post Bottom Ad