
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Bw. Selestin Gesimba (kulia) akiwa na Meneja Mkuu wa Multchoice Tanzania,Bw. Peter Fauel (kushoto) na Kaimu mkuu wa shule ya Sekondari ya Jangwani Mama Ruteganya wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kituo cha kurushia vipindi mbalimbali vya DSTV kwa ajili ya mafunzo kwa wanafunzi wa shuleni hapo.Multchoice imeshaanzisha vituo kama hivyo katika mikoa mbalimbali hapa nchini ikiwemo Morogoro,Mbeya,Iringa na Arusha.

Meneja Masoko wa Multchoice Tanzania,Furaha Samalu (kushoto) akiongea na Meneja uhusiano wa kampuni hiyo,Barbara Kambongi.

Wanafunzi wakiwa wamepozi kwa picha mara baada ya king'amuzi hicho kuzinduliwa rasmi leo.

Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Jangwani wakiimba wimbo maalum mbele ya wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa king'amuzi cha kurushia vipindi mbalimbali ya DSTV yanayotoa elimu na mambo mbalimbali kwa wanafunzi, king'amuzi hicho kimefungwa na kampuni ya Multchoice.picha na Full Shangwe Blog.
No comments:
Post a Comment