HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 10, 2010

Afrika Mashariki Kuunganishwa Kwa Reli

Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mshariki, Balozi Juma Mwapachu akiongea na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa Reli kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia kesho tarehe 11th -12th , Machi.Dhima kuu ikiwa ni Uendelezaji wa mfumo wa usafiri wa reli kwa lengo la kudumisha ushirikiano, kurahisisha usambazaji wa bidhaa na kukuza chumi za Jumuiya ya Afrika Masharikai na zile za SADC na COMESA
Katibu Mkuu, Wizara ya Miundombinu,Injinia Omar Chambo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu uimarishaji wa miundombinu ya reli katika Jumuiya ya Afrika Mashariki hasa ujenzi wa reli mpya kutoka Dar es salaam - Tanzania mpaka Kigali - Rwanda ambayo pia itaiunganisha nchi ya Burundi. Kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stergomena Tax.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad