
Kiongozi wa Bendi ya Machozi,Lady Jaydee akikamua stejini kama kawa

Mwinyi na Sam wakililisha vilivyo ndani ya Machozi Band katika kiota chao cha kila Ijumaa,pale Zhonghua Garden

Lady Jaydee na Machozi Band wakifanya vitu vyao usiku huu ndani ya kiota cha Zhong Hua Garden.kila Ijumaa bendi hii ya Machozi hufanya makamuzi ya kufa mtu katika kiota hiki.

Kapten Gardener G. Habash akichezesha mchezo wa bahati nasiku ya Vocha ya Zantel kwa mtu yeyote ambae angekuwa wa kwanza kuziingiza namba hizo

hapa kila mtu alikuwa akisikiliza kwa makini namba hizo wakati zinatajwa ili aweze kushinda vocha hiyo.kuna jamaa ambae ndie alieshinda lakini kwa bahati mbaya picha yake haikuweza patikana.

Mtarimbo ukizungushwa kwa uongozi maridadi kabisa toka kwa mwimbaji wa Machozi Band,afahamikae kwa jina la Mwinyi.
No comments:
Post a Comment