HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 16, 2010

Hepi Besdei Ya Kuzaliwa Mtoto Diana John Bukuku

Mtoto Diana John Bukuku (kulia) akishirikiana vyema kabisa na rafiki yake Grolia Msechu kukata keki wakati wa hafla ya kusherehekea Hepi Besdei ya kutimiza miaka 8 ya kuzaliwa kwake iliyofanyika nyumbani kwao Temeke karibu na Viwanja vya maonyesho ya Biashara vya Saba Saba jijini Dar es salaam jana jioni.Familia ya Bw. John Bukuku a.k.a Mzee wa Full Shangwe Blog inampongeza sana mtoto wao mpendwa na inamtakia maisha marefu na mafanikio katika masomo yake mungu ambariki sana Mtoto Diana John Bukuku.
Mtoto Diana John Bukuku akimlisha keki dada yake Ivone wakati wa hafla yake ya Hepi Besdei ya kuzaliwa iliyofanyika nyumbani kwao Temeke karibu na Viwanja vya vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu J.K.Nyerere a.k.a Saba Saba jijini Dar jana jioni .Hongera Mtoto Diana John Bukuku kwa kutimiza miaka 8. taslimu na bila chenji kubaki ya kuzaliwa kwako na Mungu akibariki sana na akujaalie afya njema pia.

1 comment:

  1. Hongera saana "Uncle" D.J.B.
    Pole na hongera kwa wazazi na walezi wote walioshiriki kukusaidia kufikia hapa ulipo.
    Blessings

    ReplyDelete

Post Bottom Ad