HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 18, 2009

Mubarak Ngombo Na Zakhia Kapalata Wameremeta

bwana harusi Mubarak na bi harusi Zakhia wakipozi mbele ya kekizz
bwana na bibi harusi,pamoja na wapambe wao wakigonga chiazz kwa furaha na amani tele
maharusi wakiwa meza kuu ya hai tebo kwa raha zao
mzee wa MTAA KWA MTAA akiendeleza libeneke la utambulisho katika mnuso huo ulifanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Sunset holi uliopo kule Mbezi bichi.(suti za kuazima kumbe huwaga zinamtoa chicha kweli huyu mzee wa Mtaa Kwa Mtaa,haha ahaha haha)
mambo yalianzia ukumbi wa shule ya mnazi mmoja holi ambapo ndipo ndoa ilipofungwa
Bi harusi Zakhia akiwaatika pozi na Dada yake afahamikae kwa jina la Amina Kapalata
chiazz zikiendelea kwa upande wa wazazi wa pande zote mbili.
bi harusi aliomba kupata picha ya ukumbusho na Mzee wa Mtaa Kwa Mtaa pamoja na wadau wengine katika sherehe ya harusi iliyofanyika usiku wa kuamkia leo.

siku zote mwisho wa sherehe ni lazima watu wayarudi magoma,na hapa ndio mambo yamekolea.MTAA KWA MTAA inawatakia kila la kheri katika maisha yenu ya ndoa Bwana Mubarak na bi Zakhia,na mungu awajaalie zaidi na zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad