



Wengi tunadhani Michael Jackson amefika tamati lakini ukweli ni kuwa ndio kwanza ameanza. Mchana wa leo anakutana na Mahtma Gandhi ili kupata muongozo wa namna ya kuishi vyema katika ulimwengu wa roho, jioni anakutana na Bob Marley kwa ajili ya kupiga show ya kumkaribisha huko. Kwenye majira ya saa tatu usiku atapitiwa na Princess Diana akiwa na Mama Theresa ili kupelekwa kwenye kilabu cha wenye roho za kusaidia wenye matatizo.
Ukweli ni kwamba Michael anaishi bado.
Kufa kuna raha yake kama uliishi kwa kufanya kazi uliyotumwa hapa duniani. Kitu cha kwanza kabisa unachotakiwa kufahamu ni nini hasa ulichofata hapa duniani.Kuna kazi moja tu tunayotakiwa kufanya, KUPENDA WENGINE bila ya kujali kama watarudisha upendo wao kwetu ama la!Akiwa na umri wa miaka mitano, Michael Jackson alipanda jukwaani akiwa na kundi la Jackson 5 na kutikisa anga la muziki kwa kukonga nyoyo za wapenzi wengi wa fani hiyo, wakiwa na vibao kadhaa lakini kile kilichowahi kunikaa akilini zaidi ya vingine ni "I'll be There".
Mwanzoni mwa miaka ya 80 Michael akaamua kuachana na kundi lake la Jackson 5 na kuanza kupiga muziki kwa kujitegemea. Albamu yake ya Thriller aliyotoa mwaka 1983 inasemekana ndio albamu iliyouza kuliko zote katika anga za Muziki, ikiwa imeuza nakala zaidi ya milioni 100 na ikiwa pia imebeba nyimbo saba ambazo zote ziliwahi kushika nafasi ya kwanza katika anga la muziki. Huwezi kufikia mafanikio haya kama moyo wako hauna mapenzi kwa kile unachokifanya na wale unaofanya kwa ajili yao.
Michael alikuwa ni mwanadamu wa kawaida na hakukosa mapungufu, alipenda sana watoto kwa mfano hadi kujikuta akiingia kwenye utata wa kuwafanya vibaya watoto wa watu lakini baadae ikaja kuthibitika kuwa alizushiwa. Wako waliodai alishinda mashitaka yale kwa sababu ya umaarufu wake.Wako ambao wamekuwa wakimshutumu sana kwa kujibadili rangi ya ngozi yake na hata sura yake. alijaribu kujitetea kuwa alikuwa katika harakati za kufurahia maisha yake binafsi, kwani mwili aliokuwa akiutumia ulikuwa ni wa kwake na si wa mtu mwingine, lakini hatukutaka kumsikia wala kumsikiliza.Kwa kifupi tulimchukia kabisa Michael lakini yeye mwenyewe hakuacha kuwapenda waliomchukia na mwezi ujao alikuwa amepanga kufanya maonesho 50 ya muziki wake aliyoyabatiza jina la "This is It".
Alikuwa akitegemea kutumia maonesho haya kusafisha jina lake, kutengeneza fedha za kusawazisha uchumi wake, lakini kubwa zaidi ilikuwa ni kkidhi kiu ya washabiki wake ambao walikuwa hawajamuona siku nyingi.Habari zilizopo sasa zinasema Michael amefariki baada ya moyo wake kusimama. Swali moja linaibuka, nini kilichosababisha moyo kusimama? Jibu la haraka toka kwa wachambuzi wa mambo ni kwamba Michael anafahamika kwa kuwa mchapa kazi kupindukia, hasa mazoezi ya kucheza.
Kuna wakati alipata kuzimia baada ya kufanya mazoezi masaa kumi na nne mfululizo ili kutayarisha video yake ya Dangerous, madaktari wakamuwahi na akapona. Kwa hivyo wachunguzi wanadai huenda na safari hii hadithi ikawa ni hiyo kwani inasemekana Michael alitaka maonesho haya yawe kabambe.Uchunguzi wa kidaktari juu ya sababu hasa ya kifo hiki unatarajia kufanyika kati ya leo au kesho.taarifa hii ni kwa hisani ya FotoBaraza.Net
naona wino mwekundu inakuwa shida kusomeka mzee
ReplyDeleteKaka. Hiyo picha ya MJ akitoka mahakamani yuko na Latoya na si Janeth.
ReplyDeleteBlessings