

SHIRIKISHO LA MPIRA WA KIKAPU TANZANIA (TBF) PAMOJA NA WADAU WOTE WA MPIRA WA KIKAPU TANZANIA TUMEPOKEA KWA FURAHA KUBWA KWA MTANZANIA MWENZETU HASHEEM THABEET KWA KUCHAGULIWA KWAKE KUWA MCHEZAJI NAMBA MBILI KATI YA WACHEZAJI THELATHINI KATIKA RAUNDI YA KWANZA KUCHEZEA TIMU YA MEMPHIS GLIZZLIES.
HAKIKA JANA SAA MOJA NA DAKIKA THELATHINI NA TISA ITAKUA IMEWEKA HISTORIA KWA HASHEM NA WATANZANIA WOTE BAADA YA KAMISHNA MKUU WA NBA DAVID STERN KUMTANGAZA HASHEEM KUWA NDIO CHAGUO LA PILI AKITANGULIWA NA BLAKE GRIFFIN AMBAYE AMEENDA LA CLIPPERS NA KUWAPITA KWA MBALI WASHINDANI WAKE WALIOPEWA NAFASI ZA JUU WAKATI WA MCHAKATO DE JUAN BLAIR (37) AMBAYE AMEENDA SAN ANTONIO SPURS NA RICKY RUBIO (5) AMBAYE AMEENDA MINNESOTA.
TBF INAWAPONGEZA WOTE WALIOWEZESHA MAFANIKIO YA KIJANA WETU AMBAYE ATATULETEA SIFA NA KUITANGAZA TANZANIA, RASI WA JAMHURI WA TANZANIA KIPEKEE KWA KUMSHAURI NA KUMPA MOYO KILA WAKATI, CHAMA CHA MPIRA WA KIKAPU CHA MKOA WA DAR ES SALAAM, MAMA HASHEEM NA NDUGU ZAKE PAMOJA NA UBALOZI WA MAREKANI KWA KUTUTAARIFU MARA KWA MARA NA KUFUATILIA MAENDELEO YAKE NA KUTUPA MOYO.
MUNGU MBARIKI HASHEEM
MUNGU IBARIKI TANZANIA
LAURENCE CHEYO
KATIBU MKUU- TANZANIA BASKETBALL FEDERATION
No comments:
Post a Comment