
balozi wa uingereza nchini mh. Diane Corner akiwasha mishumaa ikiwa kama ishara ya kuifungua tawi la Man u hapa bongo,sherehe zilizofanyika katika hotel ya Regency park jana kabla ya kula kichapo cha 2-0 toka kwa timu ya Barca usiku wa kuamkia leo.

mkuu wilaya ya nanihii ndugu Issa Michuzi a.k.a Mzee wa Libeneke akipiga story na viongozi wa tawi la man u pamoja na Balozi wa uingereza katika sherehe ya uzinduzi wa tawi la chama lao hilo iliyofanika jana jioni pale Regency park.(sijui ndio alikuwa anawapa pole kwa kichapo walichokipata toka kwa Barca?maana wote wamenuna kasoro yeye tu.)

viongozi wa tawi la man u bongo,wakimpongeza Balozi wa uingereza alipokuwa akitoa maneno yake machache kwa wanazi wa timu ya man u hapa bongo.

mkuu wa itifaki wa kamati ya miss Tz ambae pia ni kiongozi katika tawi hilo la man u hapa bongo,mkuu Albert Makoye akitoa maneno mawili matatu katika mahojiano na chombo kimoja cha habari hapa bongo.kama namuona sasa hivi huko aliko maana man u ikifungwaga nafikiri hata kuumwa huwa anaumwa.

wana man u wakipongezana baada ya kuzinduliwa kwa tawi lao hapa bongo.
No comments:
Post a Comment