HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 28, 2009

barcelona ndio mabingwa wapya 2009/10

mabongwa wapwa wa klabu bingwa ulaya,Barcelona ya Hispania wakisherehekea ubingwa wao mara baada ya kuibanjua timu ya Man utd mabao 2-0,katika mechi iliyochezwa usiku wa kuamkia leo jijini Roma huko nchini Italia
mCameroon Samuel Eto'o akiipatia timu yake ya Barcelona bao la kuongoza kunako dakika ya kumi hivi na kufanya matokeo yawe 1 bin ziro.
mchezaji Lionel Messi mwenye asili ya kiArgentina akiipatia bao la pili timu yake ya Barcelona katika mechi ya fainali ya klabu bingwa ulaya na kuofanya kuwa mabingwa wapya kwa mwaka 2009/10
Tevez,Evra pamoja na baba yao Giggs wakiwa wameduwaa kwa kutoamini kwamba kombe lile kombe walilolichukua mwaka jana leo hii limeota mbawa.
raha sana kwa mchezaji wa zamani wa Arsenal,Thieri Henry maana leo ndoto yake ndio imetimia mara baada ya kulikosa miaka kadhaa iliyopita.halafu raha hii sio kwa Barca tu bali ni kwa kila mpenzi wa mpira wa miguu Duniani,na hata kina sisi pia tunafuraha maana kama wangelichukua hawa mashetani basi huku mitaani tungekoma.picha zote kutoka hapa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad