HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 29, 2009

mtikisiko ndani ya jiji la dar leo

watu wakitoka katika maofisi yao mara baada ya kupita kwa mtikisiko wenye kishindo kikubwa katika maeneo mengi ya jiji la dar mchana huu.kila mtu alitoka nje ya jengo la jm mall kutaka kujua ni kitu gani kinaendelea huko nje,bila ya kupata jibu lililo sahihi,maana wengine wanasema ni tetemeko la ardhi linapita,wengine wanasema kuna mabomu yanalipuka huko maeneo ya Mbagala nk.hizi ni baadhi ya picha tu nilizozipata sasa hivi,ila kwa uhakika zaidi tutajuzana baadae ili kujua ni kitu gani kilikuwa kinaendelea kwa wakati huo,hivyo endeleeni kukatizakatiza hapa kwa taarifa kamili.


KWA HABARI ZILIZOPATIKANA HIVI PUNDE KUTOKEA MAENEO YA MBAGALA KIZUIANI,INASEMEKANA KWAMBA GHALA NA SILAHA ZA KIJESHI LILILOPO MAENEO YA MBAGALA KIZUIANI LIMELIPUKA NA KUSABABISHA WATU KUKIMBIA MAKAZI YAO NA UHARIBIFU MKUBWA WA MAKAZI YA WATU HA PAMOJA NA KUJERUHI BAADHI YA WATU NA WENGINE KADHAA KUPOTEZA MAISHA,HII HALI IMEKUWA IKITISHIA SANA MAISHA YA WAKAZI WA JIJI NA DAR.HATA HIVYO WAZIRI WA ULINZI NA USALAMA AMEAMURU WATU WOTE WALIO KATIKA MAJENGO MAREFU KATIKATI YA MJI WAONDOKE KABISA KATIKA MAENEO HAYO KWA HALI IMEISHA KUWA MBAYA.TUTAENDELEA KUJUZANA BAADAE KINACHOENDELEA JUU YA TUKIO HILI LILILOLIKUMBA JIJI LETU LA DAR.HIVYO TUVUTE SUBIRA KIDOGO..


1 comment:

  1. mwanangu tunakuaminia mwaga picha ili tuone hali halisi ya sehemu hiyo ya jiji.tulio nje ya nchi tunafuatilia kwa makini sana.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad