
penye zali kama hili vibaka hawakosekani. hawa wamedakwa wakisaidia kuanua nguo zilizoachwa nyuma wakati wenye nazo wametoka nduki kwa mlipuko uliokuwa ukiendelea huko Mbagala leo.

watu waliofika eneo la tukio wakiangalia mabaki ya mojawapo ya mabomu yaliyoruka umbali wa kilomita nne na kutua sehemu za mbagala kizuiani. ni moja ya takriban ya mabomu 12 yaliyolipuka na kutua uraiani.

hivi ndivyo ilivyokuwa barabara ya mbagala leo

askari wa zima moto na walifika eneo la tukio lakini hawakuweza kufanya lolote kutokana na hali ilivyokuwa katika eneo hilo.

wakazi wa maeneo ya Mtoni Mtongani wakiwa juu ya daraja la mtoni wakiangalia mambo yanavyoendelea huko Mbagala.kwa picha zaidi zama
hapa
No comments:
Post a Comment