HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 3, 2009

aliekuwa shahidi muhimu katika kesi ya kina zombe,koplo rashid lema afariki dunia

Mshtakiwa wa 11 katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva teksi mmoja, yaliyotokea kipindi kirefu kidogo kilichopita hapa jijini Dar es salaam,amefariki dunia alfajiri ya leo katika hospitali ya Ocean Road, Koplo Lema ambaye alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa muda na baadae kuhamishiwa Hospital ya Ocean Road.
Koplo Lema ambaye ni shahidi muhimu sana katika kesi hiyo ambayo inawakabili watuhumiwa wengine tisa, akiwemo mshtakiwa namba moja, Abdallah Zombe, ambaye alikuwa mkuu wa upelelezi wa Dar es Salaam,Koplo Lema alilazimika kulazwa katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili akitokea katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke alikokuwa amelazwa tangu kiasi cha wiki tatu zilizopita, baada ya kusumbuliwa na maradhi ya hapa na pale kwa muda kidogo
.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad