HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 31, 2008

MASHINDANO YA KARATE KUANZA KESHO

Mwenyekiti wa Japan Karate Association Tanzania,Bw. Daniel Mbega kushoto akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya habari maelezo juu ya mashindano ya karate kwa vijana wadogo na wa kati yanayotarajiwa kuanza kesho jumamosi tarehe 1/11/2008 katika viwanja vya Don Bosco Upanga.wanaofuatia toka kulia ni David Murwa mweyekiti JKA Kenya,Jerome George wa JKA Tanzania na mmoja wa wana habari waliokuwepo kwenye mkutano huo
Mtoto Anuary Hirary kulia mwenye mkana wa Kijani akijiandaa kumpiga konde mpinzani wake Nestori Federiko wakati wa onyesho lao mbele ya waandishi wa habari.


Chama cha Japan Karate Association tawi la Tanzania kimeandaa mashindano ya mchezo wa karate  kwa vijana wadogo yanayotarajiwa kuanza jumamosi tarehe mosi Novemba mwaka huu katika viwanja vya Don Bosco Youth Centre jijini.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa idara ya habari maelezo mwenyekiti wa chama hicho nchini Daniel Mbega amesema vilabu mbalimbali vitashiriki kwenye mashindano hayo ambayo yataanza kesho jumamosi saa mbili na nusu asubuhi.

Amevitaja vilabu vitakavyoshiriki kuwa ni Scorpion Shotokan karate, Fitness one Karate, Genessis Int. School karate,Chita Karate,Nyuki Karate, Iringa A. Karate na Iringa B. Karate vya mkoani Iringa.

Ameongeza kuwa mashindano hayo yanajumuisha mapambano ya vijana wenye umri wa kuanzia miaka 5 na 6, 7 na 9, 10 na 12, 13 na 15 ambapo zawadi mbalimbali zitatolewa ikiwa ni medali na vikombe, kiingilio kitakuwa shilingi 3.000 na viti maalum itakuwa 5.000 wapenzi wote wa mchezo wa karate manakaribishwa ili kupata burudani.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad