HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, October 18, 2008

Hatua Za Mwisho Za Ziara Ya Rais Jakaya Kikwete Mkoani Mbeya

Rais Jakaya Kikwete akimpa msaada wa pesa kijana mlemavu ambaye hana mikono aliyekuwa miongoni mwa wakazi wa mji wa Mbozi walio hudhuria sherehe za ufunguzi wa tawi la benki ya CRDB Tawi la Mbozi.wa kwanza kushoto ni mke Mama Salma Kikwete.
Raisi Jakaya Kikwete akiwahutubia wakazi wa mji mdogo wa Chunya wakati alipokuwa katika ziara ya wilaya ya Chunya mkoani Mbeya. 
Mwenyekiti wa umoja wa wachimba madini wadogowadogo wilayani Chunya Bwana George Mwaikela akiteta jambo na Rais Jakaya Kikwete muda mfupi baada ya Rais kuwahutubia wananchi wa wilaya ya Chunya katika eneo la Mkwajuni wilayani humo. 
Rais Kikwete akikagua Mfereji wa Umwagiliaji mashamba ya mpunga ya wakulima wadogo wadogo huko Uturo,wilayani Mbarali jana. 
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Dr. Charles Kimei akiwatambulisha kwa Rais Jakaya Kikwete baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo baada ya Rais kikwete kufungua tawi la benki hiyo katika mji wa Mbozi 
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbarali muda mfupi kabla ya kufungua jengo jipya la halmashauri hiyo jana. Picha zote na mdau Freddy Maro wa Ikulu 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad