HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 4, 2008

Ziara Ya Rais Kikwete Mkoani Iringa

Rais Jakaya Kikwete akiongea na mfanyabishara wa Nyanya katika Soko la Igagala,Njombe, Bi Grace Shirima baada ya kufungua Soko
Rais Kikwete akiongea na watoto mapacha walioungana Maria na Consolata wakati alipotembelea Hospitali ya Kanisa Katoliki inayoendeshwa na wamissionari wa Shirika la Consolata iliyopo Ikonda Makete,Mkoa wa Iringa.Mapacha hao ambao sasa wana umri wa miaka kumi na moja( 11) hawawezi kutenganishwa kwa upasuaji kutokana sababu za kitaalamu, ni yatima ambao wazazi wao wamefariki kwa ugonjwa wa ukimwi lakini kwa bahati nzuri wao hawakuathirika na wanaendelea vizuri kiafya.Mapacha hao ambao wanahudumiwa na watawa wa Shirika la Consolata hivi sasa wanasoma darasa la tano katika shule ya Msingi Ikonda Makete na hivi sasa wanaishi nyumbani kwa Bi Betina Mbilinyi karibu na shule wanayosoma.

Rais Jakaya Kikwete akimjulia hali mtoto Desderius Mrongo mwenye umri wa miaka miwili na nusu aliyelazwa katika Hospitali ya Consolata Ikonda,wilayani Makete.Aliyembeba mtoto Desderius ni nyanya yake ambaye alimweleza Rais kuwa mama mzazi wa mtoto huyo amefariki Dunia. JK yupo Mkoani iringa kwa Ziara ya kikazi kukagua na kufungua miradi ya maendeleo

Rais Kikwete akiwahutubia wananchi wa eneo la Kilocha,wilayani Njombe jana baadaya kuzindua ujenzi wa shule ya wasichana ya Anna Makinda
Rais Jakaya Kikwete akikagua majengo ya shule ya sekondari ya wasichana ya Anna Makinda katika kijiji cha Kilocha,Ihunda, wilayani Njombe. picha/habari kwa hisani ya Blog ya jamii




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad