HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 6, 2008

Bushoke:Albamu Yangu Inafanyiwa Maujanja Zaidi China

Kutoka pande za Dom, tunamshusha kwenu Ruta Maximilian Bushoke, mchizi huyo siku chache zijazo atadondosha ‘nyu aidia’ ambayo baadae inaweza ikawa changamoto nyingine kwa wasanii waliojiajiri kupitia sanaa ya muziki wa Bongo Flava.Bushoke alitamka kwamba, albamu yake mpya ambayo tayari imeshakamilika ikiwa na jina la ‘Dunia njia’ ipo nchini China kwa ajili ya kuifanyia maujanja zaidi ikiwemo kurudufu kopi za mauzo.
“Albamu ina kazi zaidi ya kumi zikiwemo Chupa ya koka, Nimeshafika, Nimekuchagua, Angel, Dodoma, Kama, Hallo na nyingine kibao. Nataka kufanya kitu ambacho kinaweza kikawa mkombozi wetu, yaani kutengeneza kopi mwenyewe na kuzisambaza sokoni, badala ya kuwategemea wahindi kama ilivyokuwa hapo awali,” alisema Bushoke.Albamu hiyo inatarajiwa kudondoka kitaani mapema mwezi ujao.michapo hii inapatikana katika kijiji cha kaka Abdallah Mrisho.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad