HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, November 21, 2026

Serikali Yaweka Mikakati ya Kupanua Fursa kwa Vijana

 *Makamu wa Rais Kufungua maadhimisho ya mwaka mmoja wa maendeleo ya vijana nchini


Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imesema imeendelea kutekeleza programu mbalimbali zinazolenga kuwawezesha vijana kiuchumi, kijamii na kuwajengea uwezo wa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka, amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya mwaka mmoja ya mafanikio ya vijana yatakayohusisha taasisi mbalimbali za Serikali.

Amesema maadhimisho hayo yatafanyika Novemba 23, mwaka huu, katika Ukumbi wa Super Doll, Dar es Salaam, na kufunguliwa na Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi.

Nanauka amesema maadhimisho hayo yatakuwa fursa ya kuonesha mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka mmoja, ikiwemo shughuli mbalimbali zinazofanywa na vijana ambazo zimekuwa chachu ya kujiajiri na kuunda ajira kwa wengine.

Amesema katika kipindi hicho, Ofisi ya Maendeleo ya Vijana imepiga hatua katika kuratibu na kusimamia utekelezaji wa programu zinazolenga kuwawezesha vijana kiuchumi, kijamii, pamoja na kuwajengea uwezo wa kushiriki katika shughuli za maendeleo ya taifa.

Ameeleza kuwa afua zilizotekelezwa zimejikita katika uwezeshaji wa vijana kiuchumi, malezi na makuzi, elimu ya uraia na uzalendo, pamoja na kuimarisha uratibu na ushirikiano na wadau mbalimbali wa maendeleo ya vijana nchini.

Aidha, amesema maadhimisho hayo yatatoa fursa ya kuonesha misingi iliyowekwa katika kuimarisha mifumo ya uratibu, ushirikishwaji na uwezeshaji wa vijana, huku yakibainisha vipaumbele vya utekelezaji wa majukumu kwa kipindi kijacho.

Amesema hatua nyingine muhimu iliyofikiwa ni kuanzishwa kwa mifumo inayolenga kurahisisha upatikanaji wa taarifa, huduma na fursa kwa vijana, ikiwemo Mfumo wa Uwezeshaji Vijana (Youth Empowerment System – YFS), ambao katika kipindi cha majaribio umefanikiwa kusajili vijana 110,155 kabla ya kuzinduliwa rasmi.

“Katika mfumo wa uwezeshaji wa vijana, ofisi inalenga kurahisisha upatikanaji wa taarifa za huduma na fursa zinazotolewa na Serikali pamoja na wadau, na kuwaunganisha vijana na taasisi zinazotoa huduma hizo,” amesema.

Vilevile, amesema katika maadhimisho hayo kutazinduliwa Mfumo wa Uratibu wa Maendeleo ya Vijana utakaowezesha taasisi za Serikali na wadau kupanga, kutekeleza na kufuatilia kwa pamoja programu za maendeleo ya vijana.

Amesema maadhimisho hayo yenye kaulimbiu ‘Mwaka Mmoja, Vijana Pamoja’ yatahusisha maonesho ya bidhaa, huduma na ubunifu wa vijana, pamoja na ushuhuda wa vijana walionufaika na fursa mbalimbali za uwezeshaji.

Fursa hizo ni pamoja na mitaji, mikopo, zabuni za Serikali, kilimo cha umwagiliaji, ufugaji wa samaki na shughuli za viwanda.ki na shughuli za viwanda

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad