Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Ngwaru Jumanne Maghembe (Mb.), amezindua kitabu “Saint Francis of Assisi in Tanzania: A Living Presence – Mtakatifu Fransisko wa Asizi: Uwepo Ulio Hai Tanzania”, akieleza kuwa ni nyenzo muhimu ya kuhifadhi historia na mchango wa Wafransiskani katika maendeleo ya Tanzania, hususani katika elimu, afya na huduma za kijamii.
Hafla ya uzinduzi ilifanyika tarehe 2 Oktoba 2026 katika ukumbi wa Padre Pio Shrine Pastoral Centre, Msimbazi, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 800 tangu kifo cha Mtakatifu Fransisko wa Asizi.
Kitabu hicho kinaelezea historia ya Wafransiskani pamoja na mchango wao katika kuleta maendeleo ya jamii nchini Tanzania.
Akizungumza katika hafla hiyo Mhe. Maghembe amesema Tanzania inathamini mchango wa Wafransiskani katika kuleta maendeleo ya jamii na amesisitiza dhamira ya Serikali ya kuendelea kushirikiana na taasisi za dini katika utoaji wa huduma na kuimarisha ustawi wa wananchi, huku historia ya Wafransiskani ikiendelea kuwa sehemu muhimu ya urithi wa Tanzania.
Uzinduzi huo pia umeangazia nafasi ya urithi wa Wafransiskani katika kujenga madaraja ya urafiki na kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Italia, kupitia uhusiano wa watu na taasisi katika nyanja za kijamii, kiutamaduni na maendeleo.
Naye Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mhe. Giuseppe Coppola, alieleza kuwa kitabu hicho kinaonesha namna urithi wa Mt. Fransisko ulivyojenga daraja la urafiki wa kindugu kati ya Tanzania na Italia, pamoja na kuonesha mchango wa familia ya Wafransiskani katika maendeleo ya kijamii na kiutamaduni nchini.
Kwa upande wake, Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Mhe. Nicole Providoli, alieleza historia ya Wafransiskani kutoka Uswisi waliofika Tanganyika mwaka 1921 na mchango wao katika sekta za elimu, afya na maendeleo ya jamii.
.jpeg)
.jpeg)





.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
No comments:
Post a Comment