Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Letshego Faidika Bank Tanzania Limited (LFB) imezindua kampeni ya kukuza amana iitwayo “Weka. Tukuwekee!”, inayolenga kuwahamasisha Watanzania kuongeza akiba na kutumia huduma rasmi za kibenki.
Kampeni hiyo itakayodumu kwa wiki 12, imeanza tangu Oktoba 5 na inatarajiwa kumalizika Desemba 27, 2026, ikiwa inatekelezwa katika kanda tano nchini ambazo ni Kanda, Kati, Kusini, Magharibi, Ziwa na Kaskazini.
Kupitia kampeni hiyo, benki imeandaa zawadi mbalimbali kwa wateja wanaoweka fedha katika akaunti zao za “LetsGo “, huku washindi wakipatikana kila wiki na kila mwezi.
Wateja watagawanywa katika makundi matatu kulingana na kiasi cha fedha wanachoweka, ambapo mteja atakayekuwa ameweka kiasi kikubwa zaidi katika kundi lake atakuwa mshindi wa wiki.
Katika kundi la “Wathubutu”, linalohusisha wanaoweka hadi Sh50,000, mshindi wa wiki atapata Sh50,000.
Kundi la “Wajenzi”, linalohusisha wanaoweka kati ya Sh50,000 na Sh500,000, mshindi atapata Sh100,000, huku kundi la “Wakubwa”, kwa wanaoweka zaidi ya Sh500,000, mshindi akipata Sh200,000.
Mbali na zawadi hizo, kila mwezi mteja atakayekuwa ameweka fedha nyingi zaidi katika kipindi husika atashinda bodaboda mpya.
Mwisho wa kampeni, mteja mwenye jumla kubwa zaidi ya amana katika kipindi chote atazawadiwa “guta la mizigo”.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Letshego Faidika Baraka Munisi, alisema mpango huo unalenga kufanya uwekaji akiba kuwa rahisi na wenye manufaa kwa Watanzania.
“Kampeni ya Weka. Tukuwekee! ni ahadi yetu ya kufanya uwekaji akiba uwe rahisi, wenye thamani na wa karibu kwa kila Mtanzania. Tunapanua njia za kuweka pesa na kupeleka huduma zetu moja kwa moja kwenye jamii,” alisema.
Katika kuimarisha upatikanaji wa huduma hizo, benki imesema wateja wanaweza kuweka fedha kupitia matawi na vituo vya LFB, mawakala wa benki hiyo, pamoja na mitandao ya simu ya M-Pesa, Airtel Money, Tigo Pesa na HaloPesa.
Wateja pia wanaweza kuhamisha fedha kutoka benki nyingine kwenda kwenye akaunti zao za LFB. Kwa mara ya kwanza, wateja wa LFB wanaweza pia kuweka fedha kupitia mawakala wa CRDB na matawi ya TCB, huku fedha hizo zikiingia moja kwa moja kwenye akaunti zao za LFB bila makato ya ziada.
Benki hiyo inatoa aina nane za akaunti za akiba ambazo ni LetsGo Personal, Business, Flex Business, Mjasiriamali, Flex Dunduliza, Kids, Group na Mstaafu.
Kwa mujibu wa benki hiyo, akaunti ya Flex Dunduliza inatoa riba ya hadi asilimia 10 kwa mwaka, huku akaunti zote zikiwa sehemu ya kampeni hiyo.
Wateja wapya wanaweza kufungua akaunti ndani ya dakika tano kupitia “LetsGo App”, huku magari maalumu ya kampeni yakizunguka maeneo mbalimbali kuwafikia wananchi na kutoa huduma za ufunguaji akaunti, utoaji na uanzishaji wa kadi papo hapo.

Afisa Mkuu Mtendaji wa benki ya Letshego Faidika, Baraka Munisi (katikati), akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya wiki 12 ya kuhamasisha uwekaji wa akiba iliyopewa jina la “Weka. Tukuwekee!”, inayowapa wateja fursa ya kushinda zawadi za fedha kila wiki, bodaboda kila mwezi na zawadi kuu ya bajaji ya mizigo. Kulia ni Mkuu wa Biashara wa benki hiyo, Eddie Mhina na kushoto ni Meneja Uhusiano Wateja wa Kuweka, Neema Soka.
Meneja Uhusiano Wateja wa Kuweka wa benki ya Letshego Faidika Neema Soka (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya wiki 12 ya kuhamasisha uwekaji wa akiba iliyopewa jina la “Weka. Tukuwekee!”, inayowapa wateja fursa ya kushinda zawadi za fedha kila wiki, bodaboda kila mwezi na zawadi kuu ya bajaji ya mizigo. Wa pili kulia ni Afisa Mkuu Mtendaji wa benki ya Letshego Faidika, Baraka Munisi na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Biashara wa benki hiyo, Eddie Mhina. Wa kwanza kushoto ni Meneja Amana na Mtandao wa Matawi wa benki hiyo Martine Mosha,
Mkuu wa Biashara wa benki ya Letshego Faidika, Eddie Mhina (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya wiki 12 ya kuhamasisha uwekaji wa akiba iliyopewa jina la “Weka. Tukuwekee!”, inayowapa wateja fursa ya kushinda zawadi za fedha kila wiki, bodaboda kila mwezi na zawadi kuu ya bajaji ya mizigo. Pia katika picha ni Afisa Mkuu Mtendaji wa benki ya Letshego Faidika, Baraka Munisi..jpeg)
Meneja Amana na Mtandao wa Matawi wa benki ya Letshego Faidika Martine Mosha akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya wiki 12 ya kuhamasisha uwekaji wa akiba iliyopewa jina la “Weka. Tukuwekee!”, inayowapa wateja fursa ya kushinda zawadi za fedha kila wiki, bodaboda kila mwezi na zawadi kuu ya bajaji ya mizigo.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Letshego Faidikia, Kenneth Misigaro (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya wiki 12 ya kuhamasisha uwekaji wa akiba iliyopewa jina la “Weka. Tukuwekee!”, inayowapa wateja fursa ya kushinda zawadi za fedha kila wiki, bodaboda kila mwezi na zawadi kuu ya bajaji ya mizigo. Kushoto ni Meneja Amana na Mtandao wa Matawi wa benki ya Letshego Faidika Martine Mosha.
Meneja wa mikopo wa Benki ya Letshego Faidikia Gloria Maige (wa kwanza kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya wiki 12 ya kuhamasisha uwekaji wa akiba iliyopewa jina la “Weka. Tukuwekee!”, inayowapa wateja fursa ya kushinda zawadi za fedha kila wiki, bodaboda kila mwezi na zawadi kuu ya bajaji ya mizigo. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Baraka Munisi na katikati ni Mkuu wa Biashara wa benki ya Letshego Faidika Eddie Mhina

No comments:
Post a Comment