HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 17, 2026

Wiki ya Ubunifu yazinduliwa Dar, kuangazia DIRA 2050

 



WIKI ya Ubunifu Tanzania 2026 (IWTz2026) imezinduliwa rasmi, ikiashiria mwanzo wa uhamasishaji wa kitaifa wa wavumbuzi, wajasiriamali, watunga sera, wawekezaji, watafiti, washirika wa maendeleo, watendaji wa sekta binafsi na wadau wengine siku chache kablaya jukwaa kuu la uvumbuzi nchini Tanzania.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dk. Tausi Kida alisema Toleo la 2026 linakuja wakati muafaka, Tanzania ikiwa inaingia katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050 (DIRA 2050).

“Kauli mbiu ya mwaka huu inaonyesha hitaji lakusonga mbele zaidi ya matarajio kuelekea suluhisho kwa vitendo, ushirikiano na uwekezaji unaoweza kutafsiri uvumbuzi katika maboresho yanayoweza kupimika katika tija, ajira, ushindani, utoaji wa huduma za umma na ubora wa maisha,” aliongeza.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, mfumo wa ikolojia ya uvumbuzi Tanzania umekua kwa kiasi kikubwa, ukichangiwa na shughuli zinazokua kwa haraka katika maeneo ya ujasiriamali, teknolojia za kidijitali, utafiti na maendeleo, uvumbuzi wa kifedha, biashara zinazoongozwa na vijana na ushirikiano kati ya taasisi za umma na binafsi.

Alipongeza waandaaji kwani Wiki ya Ubunifu Tanzania ambayo imekuwa ikifanyika tangu mwaka 2015, imekua mojawapo ya majukwaa makubwa zaidi ya wadau wengi nchini yaliyojitolea katika maendeleo kupitia uvumbuzi.

Wiki ya Ubunifu Tanzania 2026, itafanyika kuanzia tarehe 31 Agosti hadi 4 Septemba 2026 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam,chini ya kaulimbiu; ‘Kutoka Matarajio hadi Mabadiliko: Kubuni Njia ya Tanzania kuelekea Ustawi Jumuishi;’

Naye Mwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania, Bw. Shigeki Komatsubara alisema Jukwaa hili linaunganisha taasisi za serikali, washirika wa maendeleo, mashirika ya Umoja wa Mataifa, wasomi, taasisi za utafiti, taasisi za fedha, wawekezaji, viongozi wa sekta binafsi, wavumbuzi, wajasiriamali, mashirika ya vijana, asasi za kiraia na wataalamu wa teknolojia ili kubadilishana maarifa, kutafuta suluhisho, kujenga ushirikiano na kuchangia ajenda ya uvumbuzi hapa nchini.

Alitoa wito kwa wadau kuchunguza jinsi mawazo mapya, teknolojia, utafiti, ujasiriamali, fedha na ushirikiano wa kimkakati vinavyoweza kuchangia katika utekelezaji wa DIRA 2050 ili kuharakisha maendeleo jumuishi na endelevu.

Meneja wa Programu ya Funguo ambayo iko chini ya UNDP, Bw. Joseph Manirakiza, alisema Wiki ya Ubunifu mwaka huu itatumika kama jukwaa shirikishi litakalotumika kubadilisha mawazo mbalimbali ya washiriki kuwa nyenzo ya ushirikiano, uwekezaji na suluhisho kwa vitendo katika kukuza maendeleo ya nchi.

Aliongeza kuwa programu hiyo pia itatoa nafasi ya mazungumzo na ubadilishanaji wa maarifa, maonyesho ya uvumbuzi, majadiliano ya kimkakati, mitandao na ushirikiano miongoni mwa watendaji kutoka maeneo yote ya mfumo wa ikolojia ya uvumbuzi Tanzania.

“Uzinduzi rasmi pia unaashiria kuanza kwa shughuli za usajili wa washiriki wa Wiki ya Ubunifu Tanzania kwa mwaka huu, ambapo wavumbuzi, wajasiriamali, watafiti, wawekezaji, watunga sera, wanafunzi, watendaji wa maendeleo, mashirika ya sekta binafsi, asasi za kiraia na umma kwa ujumla wanaalikwa kushiriki katika tukio hilo la siku tano na kwamba watapata fursa ya kuchangia maarifa, suluhisho na kushiriki majadiliano yanayohusiana na maeneo ambayo ni vipaumbele vya maendeleo nchini Tanzania,” alisisitiza.

Kwa mujibu wa Bw. Manirakiza, Wiki ya ubinifu pia itaweka msisitizo maalum katika ushirikiano kati ya serikali, sekta binafsi, taasisi za maendeleo, wasomi, taasisi za fedha na jumuiya inayokua ya wavumbuzi na wajasiriamali wote hapa nchini.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad