HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 19, 2026

NBAA YAWAPIGA MSASA WANAOTARAJIA KUFANYA MITIHANI YA BODI

 MKURUGENZI Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Prof. Siasa Mzenzi, amefungua warsha ya siku moja inayowakutanisha wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi, inayofanyika ana kwa ana na kwa njia ya mtandao.


Warsha hiyo imelenga kuwajengea wanafunzi uelewa na maandalizi bora kuelekea mitihani ya Bodi, kwa kuwapatia mwongozo kuhusu mbinu za kujisomea, maandalizi ya mitihani pamoja na kuzingatia maadili ya taaluma ya Uhasibu.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo, CPA Prof. Mzenzi amesema NBAA inawathamini wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi na haitarajii kuona matokeo yasiyoridhisha. Amesema kutokana na hilo, NBAA imeanzisha mpango maalumu wa kuwaandalia wanafunzi warsha na siku maalumu za mafunzo, zitakazowasaidia kupata mbinu na uelewa wa masomo mbalimbali ili kufanya vizuri katika mitihani.

Amesema warsha hiyo pia inalenga kuwafahamisha wanafunzi kile ambacho NBAA inatarajia kutoka kwao, ikiwemo kuwa na maandalizi mazuri, weledi na kuzingatia maadili ya taaluma.

Amewataka wanafunzi kutumia fursa hiyo kuongeza uelewa, kuuliza maswali na kujifunza mbinu mbalimbali zitakazowawezesha kujiandaa kikamilifu na kufanya vizuri katika mitihani ya Bodi.
Aidha, amesema NBAA itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wanafunzi na wataalamu wanaotarajia kujiendeleza katika taaluma ya Uhasibu na Ukaguzi wa hesabu nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Prof. Siasa Mzenzi akizungumza wakati ufunguzi wa warsha ya ana kwa ana na kwa njia ya mtandao kwa wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi.
Mkurugenzi wa Huduma za Shirika kutoka NBAA CPA Kulwa Malendeja akizungumza na wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi wakati wa warsha ya ana kwa ana na kwa njia ya mtandao kwa wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi.
Mkufunzi CPA Rashid Mganwa akitoa elimu kuhusu namna ya kujiandaa na kufanya masomo ya B4, C4 pamoja na maboresho ya IFRS 10 kwa wanafunzi wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi waliokuwa wanafuatilia ana kwa ana na kwa njia ya mtandao.
Mkufunzi CPA Edison Leonce akitoa elimu kuhusu namna ya kujiandaa na kufanya masomo ya B2 na C1 kwa wanafunzi wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi waliokuwa wanafuatilia ana kwa ana na kwa njia ya mtandao.
Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, CPA Dkt. Emmanuel Christopher akitoa elimu kuhusu namna ya kujiandaa na kufanya masomo ya B1 na C3 kwa wanafunzi wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi waliokuwa wanafuatilia ana kwa ana na kwa njia ya mtandao.
Baadhi ya wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi wakifuatilia mada pamoja na kuuliza maswai kwa wakufunzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Prof. Siasa Mzenzi akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa NBAA pamoja na Wakufunzi wa wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Prof. Siasa Mzenzi akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa NBAA pamoja na wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad