HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 17, 2026

MAONESHO YA UCHUMI BUNIFU LA MASHARIKI CREATIVE ECONOMY EXPO 2026 KUANZA DAR ES SALAAM KESHO UKUMBI WA MLIMANI CITY JIJINI DAR

 





MAONESHO ya uchumi bunifu yanayoenda kwa jina la Mashariki Creative Economy Expo 2026 yanaanza  jijini Dar es Salaam kuanzia kesho tarehe 18 hadi 21 Agosti 2026, yakiwakutanisha wabunifu, wawekezaji, watangazaji, wamiliki wa haki, watunga sera na wabunifu wa teknolojia kwa ajili ya kukuza uchumi wa ubunifu barani Afrika.

Maonesho hayo yaliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya  Culture and Development East Africa (CDEA) yanalenga kuifanya sekta ya ubunifu kuwa chanzo cha fursa za biashara na uwekezaji, kupitia matumizi ya haki miliki (IP) katika muziki, filamu, fasihi, sanaa za picha, maudhui ya kidijitali na maeneo mengine.

Expo hiyo pia inalenga kujenga ushirikiano wa kimkakati na majukwaa ya habari na burudani kama Azam Max, ili kukuza simulizi za Afrika Mashariki, kuibua vipaji vipya na kuunganisha wabunifu na masoko mapana ya kikanda na kimataifa.

#MasharikiExpo2026 #UchumiWaUbunifu #CDEA #VipajiAfrika #HakiMiliki #DarEsSalaam #AfrikaMashariki

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad