HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 4, 2026

Dkt. Fatuma: NIC Insurance endeleeni kutoa elimu ya bima kwa makundi

Na Mwandishi Wetu
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Fatuma Mganga, ameitaka NIC Insurance kuendelea kutoa elimu ya bima kwa makundi mbalimbali ya wananchi, ikiwamo Mabaraza,Mabaraza ya Madiwani ya Mikoa, Mabaraza ya Wafanyakazi, wanafunzi wa vyuo, shule za msingi na sekondari, ili kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa bima.

Dkt. Fatuma amesema elimu hiyo pia inapaswa kuwafikia wakulima, hususan kuhusu Bima ya Kilimo, ili kuwasaidia kujikinga na hasara zinazoweza kusababishwa na majanga na kulinda uwekezaji wao katika shughuli za kilimo.

Amesema hayo alipotembelea Banda la NIC Insurance katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Samwel Malecela, akisisitiza kuwa bima ni muhimu katika kuwalinda wananchi na mali zao dhidi ya hasara zinazoweza kusababishwa na majanga mbalimbali.

Kwa mujibu wa Dkt. Fatuma, wananchi kwa sasa wamekuwa wakijikita zaidi katika kilimo cha biashara kinachohitaji uwekezaji mkubwa wa fedha, hivyo ni muhimu kwao kuchukua bima ili kulinda mitaji na uwekezaji wao dhidi ya majanga yanayoweza kujitokeza.

“Wananchi sasa wanawekeza fedha nyingi katika kilimo cha biashara, hivyo wanahitaji kuwa na bima ili kulinda uwekezaji wao dhidi ya majanga na hasara mbalimbali,” amesema.

Aidha, Dkt. Fatuma amesema Madiwani wana nafasi kubwa katika kuwafikishia wananchi elimu kuhusu bima kutokana na kuwa karibu na jamii wanazoongoza.

Amesema kupitia Mabaraza ya Madiwani na majukwaa mbalimbali wanayoshiriki, elimu kuhusu umuhimu wa bima inaweza kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuwahamasisha kuchukua hatua za kulinda mali zao pamoja na shughuli zao za kiuchumi.

Ameongeza kuwa ushirikiano kati ya kampuni za bima na viongozi wa Serikali za Mitaa ni muhimu katika kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu bidhaa mbalimbali za bima, hususan zinazolenga kulinda shughuli za kilimo na uwekezaji wa wakulima.

[10:08 AM, 8/4/2026] Chalila Tg: Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt.Fatuma Mganga

akizungumza nkatika Banda la NIC Insurance kwenye maonesho ya Kilimo ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Dkt.John Samwel Malecela Jijini Dodoma

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad