Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Wachezaji wanaoshiriki Ligi ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) wanatarajiwa kunufaika na uwekezaji wa mwaka mmoja wenye thamani ya Sh588.9 milioni katika msimu wa 2026.
Kwa mujibu wa mkataba uliosainiwa juzi kati ya kampuni ya michezo ya kubashiri ya betPawa kwa ajili ya kuongeza udhamini kwa msimu mmoja, wachezaji watalipwa fedha hiyo kupitia mpango wa Locker Room Bonus (LRB) unaolenga kuwazawadia timu zinazoshinda.
Kupitia makubaliano hayo mapya, kila mchezaji wa timu itakayoshinda mechi atapokea Sh88,750 papo hapo, huku bonasi hiyo inawanufaisha makocha na maofisa wengine wa benchi la ufundi la timu husika baada ya kila ushindi.
Jumla ya wachezaji 12 pamoja na maofisa wanne wa benchi la ufundi, wakiwamo makocha wawili wa kila timu inayoshinda watanufaika na malipo hayo, hatua ambayo imelenga kuongeza thamani ya ushindi na kuhamasisha ushindani mkubwa katika ligi msimu mzima.
Meneja wa Kanda ya Kusini na Mashariki mwa Afrika wa betPawa, Bwalya Noah, alisema kampuni hiyo inaamini maendeleo ya mchezo wa mpira wa kikapu yanaanza kwa kuwekeza kwa wachezaji.
*"betPawa tunaamini mafanikio yanayopatikana uwanjani yanapaswa kuwanufaisha wale wanaoyaleta. Ndiyo msingi uliozaa mpango wa LRB. Timu inaposhinda, wachezaji na benchi la ufundi waliofanikisha ushindi huo wanapaswa kupata zawadi yao mara moja," alisema Noah.
Alisema mpango huo unatambua juhudi za wachezaji, unazawadia ubora na kuhakikisha mafanikio ya uwanjani yanageuka kuwa manufaa ya moja kwa moja kwa wahusika.
Noah alisema LRB imekua na kuwa moja ya programu kubwa za maendeleo ya michezo barani Afrika, ikinufaisha maelfu ya wanamichezo katika nchi mbalimbali zikiwamo Ghana, Uganda, Nigeria na Cameroon, huku mamia ya wachezaji wa mpira wa kikapu nchini Tanzania tayari wakinufaika na bonasi hizo.
Kwa upande wake, mratibu wa Masoko wa betPawa Afrika Mashariki, Nassoro Mungaya, alisema kampuni hiyo inatarajia ushirikiano huo kuendelea kuleta matokeo chanya katika maendeleo ya mchezo wa mpira wa kikapu nchini.
"Tunatarajia kuona matokeo mazuri ndani na nje ya uwanja. Tunataka kushuhudia mechi zenye ushindani mkubwa zaidi, klabu zenye uendeshaji bora na wachezaji wanaopata motisha ya kufanya vizuri katika kila mchezo,"* alisema Mungaya.
Alisema betPawa itaendelea kushirikiana kwa karibu na Basketball Dar es Salaam League pamoja na Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) kuimarisha mifumo ya uendeshaji wa ligi.
"Mbali na kulipa bonasi, tunawekeza katika kuboresha usimamizi wa ligi kupitia usajili wa wachezaji, uthibitishaji wa taarifa na uwasilishaji sahihi wa matokeo ya mechi. Mifumo imara ndiyo msingi wa maendeleo endelevu ya mchezo," alisema.
Mungaya alisema dira ya muda mrefu ya betPawa ni kusaidia kuifikisha Tanzania katika viwango vya juu zaidi vya mpira wa kikapu kwa kuendelea kuthamini ubora na kuwapa wachezaji fursa zaidi za kunufaika na vipaji vyao.
"Tunaamini kwamba wachezaji wanapotambuliwa na kuzawadiwa kwa kiwango chao, wanapata hamasa zaidi ya kufanya vizuri, klabu zinaimarika na mchezo mzima unanufaika. Huo ndiyo mwelekeo tunaotaka kuendelea kuuona nchini Tanzania," alisema.
Wakati huo huo, Rais w Chama cha mpira wa kikapu cha mkoa wa Dar es Salaam League (BDL), Shendu Hamis, alisema wanafurahia kuendelea na ushirikiano huo kwa kuwa umekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya ligi na ustawi wa wachezaji.
"Tunafurahi sana kuhuisha mkataba wetu na betPawa kwa sababu udhamini huu umeendelea kuleta thamani kubwa kwa ligi yetu. Umekuwa ukiwapa motisha wachezaji kupambana kwa nguvu katika kila mechi na umeongeza ushindani kwa timu zote msimu mzima," alisema Hamis.
Alisema mpango wa Locker Room Bonus umebadili mtazamo wa wachezaji na klabu, kwani kila mchezo sasa una umuhimu mkubwa kutokana na timu kujua ushindi unaambatana na zawadi ya kifedha.
"Udhamini huu pia umechangia kuongeza weledi katika uendeshaji wa klabu na kuinua kiwango cha ushindani wa ligi. Tunaamini ushirikiano huu utaendelea kuinua mpira wa kikapu Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla," aliongeza.
.jpeg)
Meneja wa Kanda ya Kusini na Mashariki ya Afrika wa betPawa, Bwalya Noah (katikati) akisaini mkataba wa kudhamini wa msimu wa 2026 wa ligi ya kikapu ya mkoa wa Dar es Salaam (BDL)ambapo kampuni hiyo imedhamini kwa Sh58.9m. Kulia ni Rais wa chama cha mpira wa kikapu wa Dar es Salaam (BD) Shendu Hamis na kushoto ni Mratibu wa Masoko wa betPawa Afrika Mashariki, Nassoro Mungaya.
.jpeg)
Meneja wa Kanda ya Kusini na Mashariki ya Afrika wa betPawa, Bwalya Noah (wa pili kushoto) akibadilishana mkataba wa kudhamini ligi ya kikapu ya mkoa wa Dar es Salaam (BDL) wa msimu wa 2026 na rais wa chama cha mpira wa kikapu wa Dar es Salaam Shendu Hamis(wa pili kulia). Wa kwanza kushoto ni Msimamizi wa shughuli za ofisi wa betPawa, Erick Taisamo ambapo wa pili kushoto ni mratibu wa Masoko wa betPawa Afrika Mashariki, Nassoro Mungaya na kulia ni Katibu Mkuu wa BDL, Daniel Kapongo.
.jpeg)
Meneja wa Kanda ya Kusini na Mashariki ya Afrika wa betPawa, Bwalya Noah akizungumza wakati wa kusaini mkataba wa msimu wa wa 2026 wa ligi ya kikapu ya mkoa wa Dar es Salaam (BDL)ambapo kampuni hiyo imedhamini kw Sh58.9m.
.jpeg)
Mratibu wa Masoko wa betPawa Afrika Mashariki, Nassoro Mungaya akiuzngumza katika hafla hiyo ya kusaini makataba wa msimu wa 2026 wa BDL.

Rais wa chama cha mpira wa kikapu wa Dar es Salaam (BD) Shendu Hamis akiungumza wakati wa kusaini mkataba wa msimu wa 2026 wa ligi ya BDL na kampuni ya betPawa.
.jpeg)
Meneja wa Kanda ya Kusini na Mashariki ya Afrika wa betPawa, Bwalya Noah (katikati), rais wa chama cha mpira wa kikapu wa Dar es Salaam Shendu Hamis(wa pili kulia), msimamizi wa shughuli za ofisi wa betPawa, Erick Taisamo (wa kwanza kushoto), mratibu wa Masoko wa betPawa Afrika Mashariki, Nassoro Mungaya (wa pili kushoto) na Katibu Mkuu wa BDL, Daniel Kapongo 9wa kwanza kulia) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini mkataba wa msimu wa 2026 wenye thamani ya sh588.9m.

No comments:
Post a Comment