HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 29, 2026

WAMBURA AFANYA MABADILIKO KAMANDA TABORA

 





Jeshi la Polisi Tanzania lingependa kujulisha kuwa, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura, amemhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Twaha Juma Lulengelule ambaye alikuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) Mkoa wa Tabora kuwa Kamanda wa Polisi (RPC) Mkoa wa Tabora.


Uhamisho huo umefanyika ili kujaza nafasi iliyokuwa wazi baada ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Richard George Abwao, kufariki dunia Juni 20, 2026.


Imetolewa na;

Msemaji wa Jeshi la Polisi

Makao Makuu ya Polisi

Dodoma,Tanzania

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad