HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 27, 2026

NMB, UNCDF wafungua njia mpya kwa kampuni changa za kidijitali

Benki ya NMB na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) wamesaini Hati ya Ushirikiano inayolenga kuimarisha mazingira ya kuibua, kukuza na kupanua kampuni changa zenye mawazo bunifu ya kidijitali kupitia uwezeshaji wa kisera na kisheria, masoko, mitaji na ushauri wa kitaalamu.

Makubaliano hayo yamesainiwa jijini Dar es Salaam na Afisa Mkuu wa Teknolojia na Mabadiliko ya Kidijitali wa Benki ya NMB, Kwame Makundi, pamoja na Katibu Mtendaji wa UNCDF, Pradeep Kurukulasuriya. Ushirikiano huo unaendeleza Programu ya PesaTech, iliyoanzishwa mwaka 2022 na ambayo tayari imeziwezesha kampuni changa 22 za teknolojia ya fedha.

Makundi alisema kampuni tano tayari zinafanya kazi na NMB, huku tatu zikiunganisha huduma zake katika NMB Mkononi Super App. Benki hiyo inalenga kuingiza zaidi ya kampuni changa 30 katika mfumo wake ifikapo mwaka 2030 na kuziunganisha na mitaji, masoko, wataalamu na mifumo ya kidijitali.

Kurukulasuriya alisema UNCDF inaiona NMB kuwa mshirika muhimu katika kukuza kampuni changa na kuyageuza mawazo bunifu kuwa biashara zenye uwezo wa kuongeza ajira na kutatua changamoto za wananchi
Afisa Mkuu wa Teknolojia na Mabadiliko ya Kidijitali wa Benki ya NMB, Kwame Makundi (katikati), akibadilishana Hati ya Makubaliano iliyosainiwa na Katibu Mtendaji wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Pradeep Kurukulasuriya, jijini Dar es Salaam. Makubaliano hayo yanaendeleza awamu ya tatu ya Programu ya PesaTech, itakayowezesha kampuni za teknolojia ya fedha na kampuni changa kupata ushauri wa kitaalamu, masoko na fursa za kuunganisha suluhisho zao katika mfumo wa kidijitali wa NMB. Anayeshuhudia kushoto ni Mkuu wa Miundombinu na Ushirikiano wa Kikanda katika Ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki, Paola Trevisani.



Afisa Mkuu wa Teknolojia na Mabadiliko ya Kidijitali wa Benki ya NMB, Kwame Makundi (aliyeketi kushoto), na Katibu Mtendaji wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Pradeep Kurukulasuriya, wakisaini Hati ya Makubaliano jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuendeleza awamu ya tatu ya Programu ya PesaTech, inayolenga kuimarisha mfumo wa kampuni za teknolojia ya fedha na kampuni changa za kibunifu nchini Tanzania. Anayeshuhudia katikati ni Mkuu wa Miundombinu na Ushirikiano wa Kikanda katika Ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki, Paola Trevisani, akiwa na viongozi wengine.



















No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad