Hatua hiyo imechukuliwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ikiwa ni sehemu ya operesheni ya kudhibiti wizi wa umeme na kulinda miundombinu ya shirika.
Kiongozi wa operesheni hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Usalama wa TANESCO Mkoa wa Geita, Eleutherius Katemana, amesema shirika linaendelea kuwabaini na kuwachukulia hatua za kisheria wateja wote wanaojiunganishia umeme kinyume cha taratibu na kusababisha hasara kwa shirika.
Amesema miundombinu iliyong'olewa imehifadhiwa katika Kituo cha Polisi Katoro, huku uchunguzi ukiendelea ili watuhumiwa wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Kwa upande wake, Meneja wa TANESCO Wilaya ya Katoro, Mhandisi Mohere Matenke, amewatahadharisha wananchi dhidi ya kujiunganishia umeme kwa njia zisizo halali au kupitia watu wasiokuwa na mamlaka.
Amesisitiza kuwa ofisi za TANESCO zipo wazi kutoa huduma za uunganishaji wa umeme kwa mujibu wa taratibu, na kwamba mtu yeyote atakayebainika kukiuka sheria na taratibu za uunganishaji wa umeme atachukuliwa hatua kali za kisheria.

.jpeg)


No comments:
Post a Comment