Zaidi ya wananchi 350 wamenufaika na elimu ya bima kupitia programu ya CRDB Bancassurance Caravan iliyohitimishwa leo katika eneo la Soko Kuu la Dhahabu, Geita. Kliniki hiyo ya bima kwa Kanda ya Magharibi ilizinduliwa tarehe 4 Mei 2026 mkoani Kigoma.
Programu hiyo ya CRDB Bank inalenga kutoa elimu kuhusu bima, kutembelea wateja, kutoa ushauri wa huduma za bima pamoja na kuzungumza na watumishi wa benki hiyo kuhusu huduma mbalimbali za kifedha na bima.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha kliniki hiyo, Meneja Mwandamizi wa Operesheni za Bima kutoka Makao Makuu ya CRDB Bank, Emanuel Kaganda, amesema sababu ya kuanzia katika mikoa ya Kanda ya Magharibi ni kutokana na uwepo wa shughuli nyingi za kilimo na madini. Mkoa iliyofikiwa ni pamoja na Kigoma, Tabora, Shinyanga na Geita.
Kwa upande wake, Meneja Mwandamizi wa Biashara ya Bima wa benki hiyo, Kelvin Katembo, amesema CRDB Bank ni miongoni mwa benki zinazoongoza katika utoaji wa huduma za bima nchini, huku wakitoa elimu ya bure kwa wananchi kuhusu umuhimu wa bima.
Naye Mtaalamu Mwandamizi wa Bima ya Afya kutoka Makao Makuu ya benki hiyo, Ashraf Chagulani, amesema bima ya afya ya CRDB huwasaidia wananchi kugharamia matibabu wanapougua au kupata ajali baada ya kulipia ada maalum ya bima (premium).
Kwa mujibu wa ratiba ya programu hiyo, wiki ijayo msafara wa elimu ya bima utaendelea katika Kanda ya Ziwa ambapo unatarajiwa kuanza tarehe 11 Mei 2026 mkoani Mwanza.







No comments:
Post a Comment