
ILE Fainali ya kibabe ambayo ilikuwa ikisubiriwa hii hapa ni Chelsea dhidi ya Manchester City kwenye Kombe la FA Uingereza. Kila timu inahitaji kupata ushindi siku ya leo. Je nani kuchukua Kombe hili?
Hii sio mechi ya kawaida kwa macho ya kawaida ni mechi ya hisia kali kwa pande zote mbili kwani kombe hili huenda likaleta heshima kati yao siku hii ya Jumamosi. Ni Chelsea dhidi ya Manchester City pale huku nafasi ya kuondoka na uhsindi akipewa City kutokana na ubora ambao ameonesha msimu huu.
Kwa upande wa Manchester City, huu unaweza kuwa mwisho wa enzi nyingine ya mafanikio chini ya Pep Guardiola. City wamefika fainali nne mfululizo za FA Cup, jambo ambalo hakuna timu nyingine iliyowahi kufanya katika historia ya mashindano haya. Walitwaa kombe mwaka 2023 lakini wakapoteza fainali za 2024 na 2025. Sasa wanaingia kwenye fainali hii wakitaka kuzuia fedheha ya kupoteza mara tatu ndani ya misimu minne.
Wakati kwa upande wa Chelsea wao wanaingia na maumivu tofauti kabisa. Wamepoteza fainali tatu zao za mwisho za FA Cup, na Wembley imekuwa sehemu ya mateso kwao kwa miaka ya karibuni. Takwimu zinaonyesha Chelsea wamefunga mabao manne pekee katika mechi zao nane za mwisho Wembley huku wakishindwa kufunga kwenye fainali zao nne zilizopita.
Tengeneza pesa leo kwenye michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile Keno, Aviator, Poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Takwimu zinaonesha kuwa timu hizi mbili zimekutana zaidi ya mara 180 katika mashindano yote, huku Chelsea wakiwa na ushindi 71 na City ushindi 68. Lakini kinachoumiza mashabiki wa Chelsea ni rekodi ya miaka ya karibuni.
Unaambiwa tangu Chelsea washinde fainali ya UEFA Champions League Final mwaka 2021 dhidi ya Manchester City imekuwa ngumu kwao kupata ushindi dhidi ya vijana hawa wa Pep Guardiola wakijitahidi sana ni sare.
City wameshinda mara 10 na sare tatu. Hii ndiyo longest unbeaten run ya City dhidi ya Chelsea katika historia yao hadi sasa, hivyo huu ni mchezo ambao The Blues kwa hali na mali wanahitaji kumaliza unyonge. Je wataweza kufanya hivyo leo?. ODDS KUBWA zipo hapa. Jisajili sasa.
Hata ukija kwenye suala la ubora wa sasa wa vikosi, Manchester City wanaonekana kuwa timu iliyo bora zaidi. Form yao ni nzuri sana. Katika mechi zao 23 za mwisho FA Cup, wameshinda 21. Tatizo lao kubwa limekuwa kwenye fainali pekee ambapo wanatengeneza nafasi nyingi lakini conversion rate yao hushuka vibaya. Wewe unampa nani nafasi ya ushindi?. Suka jamvi hapa.

No comments:
Post a Comment