HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 16, 2026

Benki ya Absa kuendelea kusapoti sekta ya afya nchini.

Na mwandishi wetu.

BENKI ya Absa Tanzania imesema itendelea kusapoti juhudi zenye lengo la kuboresha afya za watanzania ikienda pamoja na ahadi ya chapa ya benki hiyo isemayo ‘Stori yako ina Thamani.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi na Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Bw. Aron Luhanga wakati wa hafla ya mbio za Absa Dar City Marathon 2026 zilizoshirikisha zaidi ya wakimbiaji 3000 kutoka mikoa mbalimbali nchini jijini Dar es Salaam jana.

“Leo tumehitimisha mbio hizi za Absa Dar City Marathon kama wadhamini wakuu, sisi Absa tunasema ‘stori yako ina thamani’, tunaamini kila mtanzania, kila mwananchi ana stori ya kuandika katika maisha yake, na ukiwa huna afya njema huwezi kuandika stori hizo kwa mafanikio, na sisi tumejikita kuhakikisha watanzania wanapata afya njema.

“Kinachotokea ni kwamba, kile ambacho kimekusanywa, yale mapato yaliyokusanywa kupitia tukio hili, yanakwenda kusaidia kununua vifaa tiba kwa ajili ya wodi ya wanawake na watoto katika Hospitali ya Mnazi Mmoja”, alisema Bw. Luhanga.

Akizungumza siri ya ushindi wake, mshindi wa Mbio za Kilomita 21, Cecilia Panga kutoka Arusha alisema hii ni mara yake ya pili kushinda mbio hizo na kinachomsaidia ni kuweka bidii kubwa katika mazoezi.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam (DAA), Felix Chunga alisema Mbio za Absa Dar City Marathon zimezidi kukua mwaka hadi mwaka hii ikiwa ni mwaka wake wa sita na zimekuwa na ushiriki mkubwa kutoka kwa wanariadha kutokana na kuwa na udhamini mzuri unaotolewa na benki hiyo unaoambatana na zawadi nzuri pamoja na ubora wa taratibu za mashindano ambao pia umewawezesha washiriki wake kufanya vizuri katika mashindano ya kitaifa na kimataifa.

Katika mbio za Absa Dar City Marathon mwaka huu, washindi wa kilomita 5 upande wa wanaume ni Nicholaus Zakaria (20:08:06) na Maria Joseph (23:15:55) upande wa wanawake huku mshindi wa Kilomita 10 wanaume ni Jumanne Mnada (28:37:03) kutoka Mara na upande wa wanawake ni Anastasia Nolomongo (35:14:91), akitokea Arusha.

Kwa upande wa mbio za Kilomita 21, John Nahhai kutoka Manyara, aliibuka kidedea kwa upande wa wanaume akitumia muda wa (1:03:53:18), huku kwa upande wa wanawake, Cecilia Panga kutoka Arusha, akiondoka kifua mbele kwa kushinda mbio hizo akitumia muda wa (1:12:49:28) .
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw Obedi Laiser (kulia), akichuana pamoja na washiriki wengine wa Mbio za Kilomita 10 za Absa Dar City Marathon 2026, jijini Dar es Salaam jana. Benki ya Absa ni mdhamini mkuu wa Mbio hizo, zilizoshirikisha zaidi ya wakimbiaji 3000 kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Bernard Tesha, akishiriki Mbio za Absa Dar City Marathon 2026 pamoja na wanariadha wengine jijini Dar es Salaam jana. Benki ya Absa ni mdhamini mkuu wa Mbio hizo zilizoshirikisha zaidi ya wakimbiaji 3000 kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Mshindi wa kilomita 21 wanawake wa Mbio za Absa Dar City Marathon 2026, Bi. Cecilia Panga (kulia), kutoka Arusha, akipokea zawadi ya pesa taslimu kiasi cha shs 1,500,000 kutoka Kwa Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Aron Luhanga, mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo, jijini Dar es Salaam jana. Benki ya Absa ni mdhamini mkuu wa Mbio hizo zilizoshirikisha zaidi ya wakimbiaji 3000 kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Ofisa Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya Absa Tanzania, Oscar Mwamfwagasi (kushoto), akikabidhi zawadi Kwa mmoja wa washindi wa Mbio za Absa Dar City Marathon 2026, jijini Dar es Salaam leo. Benki ya Absa ni mdhamini mkuu wa mbio hizo zilizoshirikisha zaidi ya wakimbiaji 3000 kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Mkurugenzi wa Sheria na Udhibiti wa Benki ya Absa Tanzania, Alistides Kashasira (kushoto), akikabidhi zawadi Kwa mmoja wa washindi wa Mbio za Absa Dar City Marathon 2026, jijini Dar es Salaam leo. Benki ya Absa ni mdhamini mkuu wa mbio hizo zilizoshirikisha zaidi ya wakimbiaji 3000 kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja na Huduma za Kidigitali wa Benki ya Absa Tanzania, Samuel Mkuyu (kushoto), akikabidhi zawadi Kwa mmoja wa washindi wa Mbio za Absa Dar City Marathon 2026, jijini Dar es Salaam leo. Benki ya Absa ni mdhamini mkuu wa mbio hizo zilizoshirikisha zaidi ya wakimbiaji 3000 kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser, pamoja na wafanyakazi walioshiriki Mbio za mwaka huu za Absa Dar City Marathon, wakipozi kwa picha ya kumbukumbu mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo, jijini Dar es Salaam jana. Benki hiyo ni mdhanini mkuu wa mbio hizo.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad