Kupitia toleo hili la nne, Qualcomm inathibitisha tena dhamira yake ya kuimarisha mfumo wa teknolojia ya hali ya juu barani Afrika kupitia ushauri, mafunzo, na mipango ya kukuza miliki bunifu (IP)
Kampuni ya Qualcomm Incorporated leo imetangaza uteuzi wa kampuni changa au startups 10 kwa mwaka wa nne wa Mpango wa Ushauri wa Qualcomm® Make in Africa. Mpango huu ni sehemu ya Qualcomm Africa Innovation Platform, unaolenga kusaidia maendeleo ya mfumo wa teknolojia ya hali ya juu barani Afrika. Unatoa ushauri na mafunzo, ukiweka mkazo kwenye teknolojia za mawasiliano ya kisasa na uchakataji kama vile Edge AI/ML, kompyuta (compute), IoT (Mtandao wa Vitu), pamoja na jukwaa la maendeleo ya AI (Akili Bandia) la Qualcomm kupitia Arduino.
Mambo Muhimu:
Katika fainali ya mpango huu, kampuni changa moja itapata ruzuku kutoka Social Impact Fund ya Qualcomm for Good.
Kampuni Changa zote zitapata posho ya dola za Marekani 5,000 baada ya kukamilisha mahitaji ya mpango kwa mafanikio.
Qualcomm inatoa rasilimali mbalimbali ikiwa ni pamoja na mwongozo wa kubuni bidhaa kwenye majukwaa ya Arduino AI, ushauri wa biashara, upatikanaji wa wataalamu wa uhandisi, na elimu ya bure ya miliki bunifu kupitia L2Pro Africa.
Kwa toleo la mwaka huu la mpango huu wa kipekee wa ushauri barani Afrika usiohitaji hisa (equity-free), kampuni changa 10 za awali zilichaguliwa kutoka zaidi ya maombi 1,200 kutoka nchi zaidi ya 45 za Afrika. Uchaguzi ulizingatia uwezo wao wa kutumia teknolojia za hali ya juu za mawasiliano na uchakataji katika suluhisho bunifu za mifumo kamili. Sekta zinazowakilishwa ni pamoja na kilimo, teknolojia saidizi, miji janja, miundombinu janja, usafiri wa magari ya umeme (EV), na elimu.
Kampuni Changa za kundi la 2026 ni:
Amperra Charging Company (Namibia): Mfumo wa kuchaji magari ya umeme (EV) unaotumia AI (Akili Bandia) na kuendana na gridi ya umeme, kwa ajili ya kukuza matumizi ya EV barani Afrika
Anatsor Ltd (Nigeria): Mfumo wa kidijitali wa usimamizi wa ufugaji wa kuku unaoboresha uzalishaji na ufuatiliaji wa afya
D-Olivette Labs (Nigeria): Jukwaa la bio-intelligence linalotoa uchambuzi wa data kwa ajili ya kilimo endelevu
Mindora Corporation (Zimbabwe): Kibodi ya Braille inayobooresha upatikanaji wa teknolojia kwa watu wenye uoni hafifu
MVUTU (Jamhuri ya Kongo): Mfumo wa kuhifadhi mazao kwa baridi unaotumia nishati ya jua na IoT
QualiKeeper Investments Ltd (Zambia): Mfumo wa AIoT wa kufuatilia mifugo kwa gharama nafuu maeneo ya vijijini
SafeSip (Tanzania): Suluhisho la maji salama linalotumia teknolojia janja kwa maeneo ya mijini na pembezoni mwa miji
Sesi Technologies Ltd (Ghana): Kifaa kinachotumia AI kutathmini ubora wa kakao mapema
TWave Ltd (Uganda): Mfumo wa kulisha samaki unaotumia nishati ya jua
Zerobionic (Kenya): Suluhisho za roboti saidizi kwa watu wenye ulemavu
“Ubunifu wa kampuni changa wa mwaka huu unaonyesha ukuaji mkubwa wa mfumo wa ubunifu barani Afrika,” alisema Wassim Chourbaji, Rais wa Mashariki ya Kati na Afrika na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Masuala ya Serikali katika Qualcomm. “Kampuni changa hizi zinaonyesha uwezo wa teknolojia kama Edge AI na 5G, na jinsi zinavyoweza kutumika kwa kiwango kikubwa barani Afrika.”
Washiriki watapata majukwaa ya Arduino yenye uwezo wa edge-AI bila malipo, pamoja na ushauri wa kiufundi na biashara. Fabio Violante wa Arduino alisema kuwa vifaa kama Arduino® UNO™ Q vinawawezesha waanzilishi kubadilisha mawazo kuwa mashine janja kwa haraka.
Pia watapata msaada wa maendeleo ya bidhaa na ushauri wa kulinda miliki bunifu, ikiwa ni pamoja na msaada wa usajili wa hataza kupitia Adams & Adams na mafunzo ya IP kupitia L2Pro Africa.
Mwisho wa mpango, kampuni changa zitastahili kupata ufadhili kupitia Qualcomm for Good, pamoja na posho ya dola 5,000 kwa washiriki wote waliokamilisha mpango. Wanaowasilisha haki miliki zao wanaweza kurejeshewa hadi dola 5,000 za gharama za usajili.
Baraza la Umoja wa Mawasiliano Afrika (ATU) linaendelea kuwa mshirika kwa mwaka wa nne mfululizo. Katibu Mkuu John Omo alisema mpango huu unawezesha wabunifu wa Afrika kutumia teknolojia kutatua changamoto za Afrika.
Kwa maelezo zaidi tembelea:
https://www.qualcomm.com/
Kuhusu Qualcomm
Qualcomm ni kampuni inayobuni teknolojia za kompyuta janja na mawasiliano ili kusaidia dunia kukabiliana na changamoto mbalimbali. Kupitia majukwaa yake kama Snapdragon®, inawezesha uzoefu wa kipekee kwa watumiaji na kusaidia biashara kukua kupitia teknolojia za kisasa.
Kuhusu Arduino
Arduino ni jukwaa la wazi la vifaa na programu linalotumika kuunda miradi shirikishi ya teknolojia. Lina watumiaji zaidi ya milioni 33 duniani na linatoa suluhisho kwa IoT, vifaa vinavyovaliwa, uchapishaji wa 3D, na mifumo iliyojengwa ndani (embedded systems).





No comments:
Post a Comment