MECHI ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya PSG dhidi ya Bayern kupigwa hii leo huku kila timu ikipigiwa chapuo la kuanza vyema mechi hii. Je nani kuondoka kwa kishindo?
PSG dhidi ya Bayern ni moja ya mechi ambayo ni ya kibabe na yenye kuvutiwa inayosubiriwa kwa hamu na wanasoka wengi Duniani kwani inasemekana kuwa mechi ya kasi kutokana na mfumo wa timu zote mbili lakini pia na wachezaji ambao wapo kwenye hizo timu mbili.
Ni mechi inayobeba presha ya UEFA Champions League, jukwaa ambalo mara nyingi huamua nani hasa ni mfalme wa soka la Ulaya. Katika mazingira haya, kila kosa lina gharama kubwa, na kila ubunifu unaweza kuwa tofauti kati ya ushindi na maumivu.
Kwa upande wa PSG chini ya Luis Enrique, timu imejengwa kwa msingi wa utawala wa mpira na nidhamu ya nafasi uwanjani. Wanacheza kwa utulivu lakini kwa akili nyingi, wakijaribu kumiliki tempo ya mchezo kuanzia katikati ya uwanja.
Ukiachana mechi hiyo ya UEFA, Meridianbet inakwambia tengeneza mkwanja kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Psg wakiwa kama vinara wa ligi kule Ufaransa na mabingwa watetezi wa Kombe hili wana wachezaji wenye ubora mzuri akiwamo Vitinha ambaye amekuwa akifanya vyema eneo la katikati ya uwanja,, lakini eneo zuri zaidi kwao limekuwa mbele ya safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Ousman Dembele, Doure, Khvicha, Barcola na wengine wengi.
Kwa upande wa Bayern wao mpaka sasa wakiwa na kiwango bora sana chini ya Vicent Kompany wanatarajiwa kuingia uwanjani wakiwa na nia moja tu ya kupata matokeo ambayo yatawafanya waingia mguu mmoja Fainali.
Timu hii ina makombe 6 ya UEFA huku kombe la mwisho kuchukua ilikuwa ni msimu wa 2020 ambapo alikutana fainali na huyu huyu PSG kwahiyo ni kama historia inajirudia lakini ni kwenye Nusu Fainali. Uwepo wa wachezaji wenye uwezo mkubwa kama vile Harry Kane, Musiala, Olise, Luiz Diaz, Jonathan Tah kunawafanya waingie uwanjani kwa kujiamini haswa.
Ukiangalia hizi timu mbili yaani PSG na Bayern ni timu ambazo licha ya kuwa na safu bora kabisa za ushambuliaji, lakini ni timu ambazo kwenye upande wa mabeki imekuwa ni changamoto kwani kuruhusu mabao kwao imekuwa ni rahisi sana hivyo inaweza ikawa ni mechi yenye magoli mengi sana au laah magolikipa waamue kufanya kazi ya ziada zaidi.
Hii ni mechi ya kisasi kwa vijana wa Luis Enrique kwani mara ya mwisho walipoteza mbele ya mabingwa hawa wa BUNDESLIGA hivyo hii inaweza ikawa ni nafasi yao ya kulipa kisasi. Je ni Kompany au Enrique kuanza vyema mechi hii ya Nusu Fainali pale Parc des Princes?
Kwa ujumla kabisa mechi hii ina kila dalili ya kuwa ya wazi, yenye nafasi nyingi na mabao kutoka pande zote mbili. PSG wana uwezo mzuri wa kushambulia halikadhalika kwa Bayern lakini tofauti inaweza kuja kwenye ufanisi nani atatumia nafasi zake vizuri zaidi.


No comments:
Post a Comment