******************
Na Mwandishi wetu
MOROGORO: Watumishi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wameagizwa kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kushiriki kikamilifu katika mijadala ya kikazi, kutoa ushauri wenye tija na kuchangia mawazo yatakayochochea maboresho ya utendaji wa taasisi hiyo pamoja na Serikali kwa ujumla. Wito huo unalenga kuimarisha ushirikishwaji, uwajibikaji na kuongeza matokeo chanya katika sekta ya elimu nchini.
Agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Edith Rwiza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Tatu la Wafanyakazi wa TEA uliofanyika mkoani Morogoro, ambapo alikuwa Mgeni Rasmi akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Rwiza alisisitiza kuwa TEA ina jukumu muhimu katika kuboresha miundombinu ya elimu nchini ili kuhakikisha upatikanaji wa elimu bora kwa wote. Alieleza kuwa juhudi hizo zinaenda sambamba na utekelezaji wa mtaala mpya unaolenga kukuza umahiri, ubunifu na matumizi ya teknolojia, hivyo kuwahimiza watumishi kuwa wabunifu na wenye kujituma katika maeneo yao ya kazi.
Aidha, alibainisha kuwa kuundwa kwa Baraza la Wafanyakazi ni kielelezo cha ushirikiano mzuri kati ya Menejimenti ya TEA na chama cha wafanyakazi pamoja na uzingatiaji wa sheria za kazi. Alisisitiza kuwa, mabaraza ya wafanyakazi ni vyombo muhimu vya kisheria vinavyotoa fursa kwa watumishi kushiriki katika maamuzi ya kimkakati ya taasisi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TEA Dkt. Erasmus Kipesha akiwasilisha taarifa ya mamlaka mbele ya mgeni rasmi alisema kuwa, miongoni mwa majukumu ya Baraza hilo ni kushiriki katika maandalizi ya bajeti, kupokea na kuchambua taarifa za utekelezaji, pamoja na kutoa mapendekezo ya maboresho. Aliongeza kuwa hatua hiyo inasaidia kuwajengea watumishi uelewa mpana kuhusu mwelekeo wa taasisi.
Dkt. Kipesha alieleza kuwa, TEA imeendelea kupata mafanikio makubwa ikiwemo kuimarisha ushirikiano na wadau wa maendeleo. Katika miaka ya fedha 2023/2024 na 2024/2025, mamlaka imetekeleza miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 2.15 kwa kushirikiana na wadau wake UNICEF Tanzania, huku katika mwaka wa fedha 2025/2026 miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 8.37 ikiendelea kutekelezwa, hususan katika maeneo ya STEM (Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, na Hisabati).
Naye mjumbe kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Elimu ya Juu Taifa Dkt. Nickson Mkiramweni alisisitiza kuwa, jukumu la kuijenga taasisi ni la wafanyakazi wote hivyo kila mmoja anapaswa kufanya kazi kwa bidii, uaminifu na uzalendo. Alipongeza utendaji wa Baraza la Wafanyakazi la TEA akibainisha kuwa, linaendeshwa kwa misingi ya demokrasia na uwazi hasa katika masuala yanayohusu shughuli za mamlaka hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Dkt. Erasmus Kipesha (Kushoto) akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa Baraza la Tatu la wafanyakazi wa Mamlaka hiyo, mjini Morogoro.Kulia ni Mgeni Rasmi Dkt. Edith Rwiza.
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Tatu la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania wakifuatilia hotuba kutoka kwa mgeni rasmi Dkt. Edith Rwiza (hayuko pichani) alipokuwa anazindua baraza hilo mkoani Morogoro.
Mjumbe kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Elimu ya Juu Taifa Dkt. Nickson Mkiramweni akitoa salamu kutoka makao makuu ya chama hicho wakati wa uzinduzi wa Baraza la Tatu la wafanyakazi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, mjini Morogoro.

No comments:
Post a Comment