HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 30, 2026

Serikali Yaanza Mazungumzo na Mwekezaji Mpya Kujenga Barabara ya Haraka Dar–Chalinze

 SERIKALI imethibitisha kuwa ipo katika mazungumzo na mwekezaji mwingine kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya haraka (expressway) kutoka Dar es Salaam hadi Chalinze.


Akizungumza katika mjadala maalum kuhusu namna Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPPC) kinavyofanya kazi, Mkurugenzi wa kituo hicho, David Kafulila, alisema hatua hiyo inalenga kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa ufanisi na kwa gharama nafuu.

Alieleza kuwa Serikali ililazimika kuachana na mkandarasi wa awali baada ya kubainika kuwa gharama alizowasilisha zilikuwa mara mbili zaidi ya makadirio yaliyokubalika.

Kafulila aliongeza kuwa mchakato wa kumpata mwekezaji mpya unaendelea, huku Serikali ikiweka mkazo katika kupata mbia atakayetoa huduma bora kwa kuzingatia thamani halisi ya fedha.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad