Serengeti Breweries Limited (SBL) imezindua rasmi Serengeti Premium Apple, ikiweka historia kama kinywaji cha kwanza chenye hadhi ya juu ‘Ready-to-Drink (RTD)’ kutengenezwa hapa nchini Tanzania. Uzinduzi huu unalenga kubadili mtazamo wa soko ambalo kwa muda mrefu limetawaliwa na bidhaa za kuagiza kutoka nje ya nchi, kwa kuanzisha bidhaa ya kisasa, ya kiwango cha kimataifa, iliyobuniwa na kutengenezwa kikamilifu nchini.
Ingawa soko la vinywaji vya aina hii limekua miongoni mwa watumiaji wa mijini wanaotafuta ubora na ladha ya kisasa, ukuaji huo kwa muda mrefu umefaidisha zaidi chapa za kigeni. Serengeti Premium Apple imekuja kubadilisha simulizi hiyo. Ni hatua ya kijasiri katika kuonyesha uwezo wa viwanda vya ndani, kilichotengezwa kwa ajili ya Mtanzania wa kisasa anayependelea maisha yenye mtindo na ubora wa kipekee.“Hatua hii ni kuthibitisha kuwa vinywaji vyenye ubora wa juu na viwango vya kimataifa vinaweza na kupaswa kuwa vya ndani ya nchi,” amesema Henry Esiaba, Mkurugenzi wa Masoko na Ubunifu wa SBL. “Kwa kuwekeza katika uzalishaji wa ndani, tunaimarisha mnyororo wa thamani wa ndani, kusaidia ajira, na kuchangia malengo ya kitaifa ya uendelezaji wa viwanda, huku tukikidhi ladha na mahitaji yanayobadilika ya watumiaji wa Kitanzania,” aliongeza.
Serengeti Premium Apple ni muunganiko wa kipekee wa tunda la tufaa au ‘Apple’ yaliyoiva vizuri chini ya mwanga wa jua na kinywaji chenye mng’aro angavu na wa kipekee. Kinatoa ladha safi, iliyo na uwiano mzuri na utamu wa kiasi kinachoweza kutumika kirahisi, kikitoa uburudisho wa hali ya juu katika kila funda. Kimetengenezwa kutumika na kufurahiwa kwenye nyakati za kawaida za kila siku na kuzifanya kuwa za kipekee.
Bidhaa hii imezalishwa kutokana na utafiti wa kina kupitia maoni ya watumiaji, hususani wanawake na vijana kutoka taaluma mbalimbali. “Tulibaini kuwepo kwa kiu ya hitaji la kinywaji chenye ladha na ubora wa viwango vya juu, kilichotengenezwa ndani ya nchi na kinachoendana na utamaduni wa kisasa wa kijamii,” alisema Rhona Namanya, Mkuu wa Kitengo cha Bia na RTD wa SBL. “Serengeti Premium Apple imekuja kuziba pengo hilo. Sio tu kinywaji; ni tamko la kujiamini na kujivunia, kinachoongeza nguvu katika mkusanyiko wetu wa chapa za bidhaa zetu huku kikituwezesha kupanua zaidi wigo wa soko lenye ukuaji wa kasi,” aliongeza.
Akisisitiza hoja hiyo, balozi wa chapa hiyo Bi. Flaviana Matata alisema, “Serengeti Premium Apple inawakilisha sura mpya ya utamaduni wa kusherehekea nyakati tofauti nchini Tanzania. Inaonyesha kuwa sauti za wanawake na uzoefu wao wa pamoja ni kiini cha mtindo wa maisha ya kisasa. Najivunia kuwa sehemu ya chapa inayotetea ubora, uwezeshaji na fahari ya nchi yetu.”
Zaidi ya kuwa kinywaji, Serengeti Premium Apple imetengenezwa kimkakati kuchochea shughuli za kiuchumi za ndani kuanzia kwa wasambazaji wakubwa mpaka wauzaji wa rejareja, huku ikiweka viwango vipya vya ubora wa bidhaa zinazotengenezwa nchini. Ni kiburudisho kamili kwa Tanzania mpya ambayo ipo tayari.









No comments:
Post a Comment