HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 4, 2026

BALOZI LUVANDA AITAKA NCMC KUYAFIKIA MASOKO YA KIMATAIFA

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda amekitaka Kituo cha Taifa cha Kufuatilia Kaboni (NCMC) kuimarisha na kupanua wigo wa ushiriki wa Tanzania katika masoko ya kimataifa ya kaboni.

Amesema ushiriki huo upewe msukumo kupitia uhifadhi ya mazingira na miradi ya kaboni katika sekta zote za Uchumi wa buluu, misitu, usafirishaji pamoja na nishati mbadala.

Mhe. Balozi Luvanda ameyasema hayo leo Jumatano Machi 04, 2026 wakati wa ziara yake ya kwanza kikazi katika kituo hicho tangu kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo.

Mhe. Luvanda amesema amefafanua kuwa kituo hicho kina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Taifa kupitia kaboni hivyo ni vyema kuhakikisha inaimarisha na kujenga uwezo wa Tanzania kunufaika na masoko ya biashara hiyo.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni, Bi. Kathryn Kigaraba amesema kituo hicho kitaendelea na usimamizi wa gesi joto na biashara ya kaboni ili kuwa taaasisi muhimu katika mfumo wa kitaifa wa mabadiliko ya tabianchi na masoko ya kaboni.

Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni kimeanzishwa Kwa mujibu wa Kifungu cha 29 cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, Sura ya 191 ikiwa ni taasisi ya kimkakati ya kitaifa yenye jukumu la kuratibu shughuli zinazohusiana na na biashara ya kaboni.

Biashara ya Kaboni ni mfumo wa kiuchumi unaoruhusu uuzaji na ununuzi wa Viwango vya Kaboni ambapo lengo lake ni kupunguza gesijoto angani.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda (katikati) akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC), Bi. Kathryn Kigaraba muda mfupi baada ya kuwasili katika Ofisi za Kituo hicho zilizopo Morogoro wakati wa ziara yake ya kutembelea Kituo hicho leo Jumatano Machi 04, 2026.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe Balozi. Baraka Luvanda akisalimiana na watumishi wa Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) muda mfupi baada ya kuwasili katika Ofisi za Kituo hicho zilizopo Morogoro wakati wa ziara yake ya kutembelea Kituo hicho leo Jumatano Machi 04, 2026.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe Balozi. Baraka Luvanda akisalimiana na watumishi wa Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) muda mfupi baada ya kuwasili katika Ofisi za Kituo hicho zilizopo Morogoro wakati wa ziara yake ya kutembelea Kituo hicho leo Jumatano Machi 04, 2026.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe Balozi. Baraka Luvanda akisalimiana na watumishi wa Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) muda mfupi baada ya kuwasili katika Ofisi za Kituo hicho zilizopo Morogoro wakati wa ziara yake ya kutembelea Kituo hicho leo Jumatano Machi 04, 2026.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe Balozi. Baraka Luvanda akisalimiana na watumishi wa Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) muda mfupi baada ya kuwasili katika Ofisi za Kituo hicho zilizopo Morogoro wakati wa ziara yake ya kutembelea Kituo hicho leo Jumatano Machi 04, 2026.`````
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda akiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji Kaboni (NCMC), Kathryn Kigaraba (Katikati) na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari NCMC, Bw. Hamidu Ibrahim (kushoto) muda mfupi baada ya kuwasili katika Ofisi za Kituo hicho zilizopo Morogoro wakati wa ziara yake leo Jumatano Machi 04, 2026
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda akisaini kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kuwasili katika Ofisi za Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) muda mfupi baada ya kuwasili katika Kituo hicho zilizopo Morogoro wakati wa ziara yake leo Jumatano Machi 04, 2026.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda akizungumza jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) Kathryn Kigaraba muda mfupi baada ya kuwasili katika Ofisi za Kituo hicho zilizopo Morogoro wakati wa ziara yake leo Jumatano Machi 04, 2026.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Taifa cha UfuatiliajI wa Kaboni (NCMC), Kathryn Kigaraba akizungumza jambo wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda katika ofisi za kituo hicho kilichopo Mkoani Morogoro leo Jumatano Machi 04, 2026.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala katika Kituo cha cha Taifa cha Ufuatiliaji Kaboni (NCMC) Salum Musa akizungumza jambo wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda katika ofisi za kituo hicho kilichopo Mkoani Morogoro leo Jumatano Machi 04, 2026.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Usalama wa Taarifa, Ushauri na Utafiti wa Kituo cha Taifa cha Kufuatilia Kaboni (NCMC), Paulo Lyimo akizungumza jambo wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda katika ofisi za kituo hicho kilichopo Mkoani Morogoro leo Jumatano Machi 04, 2026.
Afisa Sheria wa Kituo cha Taifa cha Kufuatilia Kaboni (NCMC), Risper Koyi akizungumza jambo wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda katika ofisi za kituo hicho kilichopo Mkoani Morogoro leo Jumatano Machi 04, 2026.

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda akifuatilia mawasilisho ya mada mbalimbali zilizowasilisha na watendaji wa Kituo cha cha Taifa cha Ufuatiliaji Kaboni (NCMC) wakati wa ziara yake ya kutembelea ofisi za kituo hicho hicho kilichopo Mkoani Morogoro leo Jumatano Machi 04, 2026.
Naibu Katibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Taifa cha Kufuatilia Kaboni (NCMC), Kathryn Kigaraba pamoja na watendaji wa Kituo hicho wakati wa ziara yake ya kikazi katika Ofisi za Kituo hicho Mkoani Morogoro leo Jumatano Machi 4, 2026.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad